Misri wavutiwa na miradi ya PPP ya TANROADS
Misri
wavutiwa na miradi ya PPP ya TANROADS
BALOZI wa Misri nchini
Tanzania, Sherif Abdelhamid amevutiwa na miradi itayojengwa kwa ubia wa kati ya
sekta binafsi na umma (PPP) itakayokuwa chini ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS),
imeelezwa.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS,
Mhandisi Mohamed Besta amesema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa
mazungumzo na Balozi huyo yaliyofanyika Makao Makuu ya TANROADS jijini Dar es
Salaam.
Mha. Besta amesema Balozi
huyo ameahidi kushiriki fursa zinazopatikana kwenye miradi ya TANROADS na
ameonesha dhamira ya makampuni ya Misri kuja kushiriki kwenye miradi ya PPP, ikiwemo
ya barabara ya kulipia ya kutoka Kibaha, Chalinze
hadi Morogoro; na Barabara za Mzunguko za Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam
Outer Ring Roads).
Miradi
mingine ya PPP ni Daraja la Pili la Kigamboni; Barabara ya kulipia ya kutoka Morogoro hadi Dodoma
na barabara ya kutoka Igawa
hadi Tunduma.
“Kama alivyosema hizi ni
mojawapo ya fursa na uzoefu
wa Kimataifa unaonesha kuwa kuna Serikali nyingi Duniani zimefanikiwa kukuza
uchumi wao baada ya kushirikisha Sekta
Binafsi katika kuboresha baadhi ya huduma muhimu za kijamii zilizopaswa
kutolewa na Serikali kwa mikataba maalum, na mfano mzuri ni nchi hizo ni
Vietnam, » amesema Mha. Besta.
Mha. Besta amesema pia katika mazungumzo yao wameweza kuainisha maeneo
ya mashirikiano katika kuendeleza sekta ya ujenzi na utaalamu wa miundombinu ya
barabara na madaraja nchini.
Amesema wamekubaliana ni namna gani Misri wanaweza kushiriki katika kuwajengea
uwezo watalaam wa TANROADS kwa kutoa mafunzo maalum na kukubali washiriki
kwenda kutembelea Misri kwa ajili ya kujifunza zaidi kutokana na maendeleo
waliyoyapata.
‘ »Tunashukuru pamoja na mazungumzo kuwa mafupi yenye lengo la
kufahamiana na kujenga mashirikiano, wenzetu wa Misri watakuja tena kuangalia
soko la ujengaji wa miundombinu ya barabara » ‘ amesema Mha. Besta.
Pia amesema Balozi Abdelhamid amefurahishwa na ujenzi wa bwawa la Umeme
la Mwl Nyerere, ambalo linajengwa na Kampuni ya Arabs Contractors ya kutoka
Misri.
Maoni
Chapisha Maoni