Pinda akerwa na ushirikina, dawa za kulevya
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewaomba viongozi wa dini nchini kuitumia mikutano ya mahubiri kutoa elimu kwa waumini wao na wananchi kwa ujumla kuachana na imani za kishirikina za kukata viungo na kuwaua walemavu wa ngozi (albino ). Pia, amewaomba kutumia mahubiri hayo kutoa elimu juu ya athari za dawa za kulevya kwa waumini wao na Watanzania wote kwa ujumla. Pinda alitoa wito huo jana wakati wa ibada ya uzinduzi wa Kanisa la Moravian Tanzania, Jimbo la Mashariki uliyofanyika kwenye makao makuu ya jimbo hilo, Mbagala Chamazi. Jimbo hilo linajumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani. Akizungumza mbele ya viongozi hao wa dini kutoka ndani na nje ya nchi, Pinda alisema Tanzania bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya matumizi ya dawa za kulevya hasa kwa vijana. “Nchi yetu imekuwa ikitajwa kwamba inatumika kwa kasi katika kusafirisha dawa za kulevya. Ni jana tu tumesikia taarifa katika vyombo vya habari zikitaja kwamba meli...