Raia wapinga mauaji ya washukiwa Garissa
Wakaazi wa mji wa Garissa nchini Kenya ambapo kulikuwa na shambulizi la kigaidi mwezi uliopita wamevishtumu vikosi vya usalama kwa kuwaua washukiwa wa ugaidi.
Wakaazi hao wanasema kuwa baadhi ya raia wametoweka baada ya kukamatwa na maafisa wa usalama.
Miili kumi na moja ilipatikana katika kaburi moja la jumla karibu na mji wa kazkazini mashariki wa Mandera mapema wiki hii.
Kundi la wapiganaji la Alshabaab lilikiri kutekeleza shambulizi hilo katika chuo kikuu cha Garissa,ambapo liliwaua karibia watu 150.
Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa lake linakabiliwa na changaoto nyingi za usalama na kwamba serikali itafanya kila iwezalo ili kuhakikisha kuwa kuna usalama
Maoni
Chapisha Maoni