Waandalizi wa maandamano waonywa Burundi
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameonya kuwaadhibu vikali wote wanaopanga maandamano ya raia dhidi yake.
Kwenye hotuba aliyowasilisha kupitia kituo cha radio ya serikali, siku ya Leba Dei, Kiongozi huyo amesema serikali itaweka vikwazo vikali dhidi ya wale aliowataja kama waasi.
Aidha amesema jopo maalum la mahakama limeundwa kuchunguza maandamano ambayo yameingia siku ya sita sasa.
Waandamanaji wanapinga hatua ya Rais huyo kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji Nchini Burundi |
Maoni
Chapisha Maoni