Maandamano mapya Baltimore Marekani
Kumetokea maandamano mapya nchini Marekani katika mji wa Baltimore kufuatia kifo cha kijana mweusi Freddie Gray aliyekufa kutokana na majeraha akiwa mikononi mwa polisi. Mamia ya watu wameandamana katika mitaa, wakionyesha ujasiri licha ya hali mbaya ya hewa iliyokuwepo.
Matokeo ya mwanzo ya uchunguzi wa polisi wa jinsi kijana wa miaka ishirini na mitano mwenye asili ya weusi alivyouawa bado hayajawekwa hadharani.Mtetezi wa haki za binadamu, Mchungaji Al Sharpton, ameitisha mkutano mjini Baltimore ili kuimarisha uhusiano baina ya polisi na wanajamii.
Maandamano Baltimore |
Maoni
Chapisha Maoni