Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2015

Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi sekondari wilayani kibondo na Kakonko mkoa wa Kigoma wameeleza wasiwasi wao kushindwa kufanya vizuri katika masomo na kukosa ajira baada ya kuhitimu pale serikali ilipotangaza kuwa kuanzia mwakani luga itakayotumika kufundishia itakuwa ni kiswahili badala ya kiingereza tangu shule za awali hadi vyuo vikuu hapa nchini

Picha
Wanafunzi wa shule ya sekondari Tutuba wakiwa Darasani Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi  sekondari wilayani kibondo na Kakonko mkoa wa Kigoma wameeleza wasiwasi wao kushindwa kufanya vizuri katika masomo na kukosa ajira baada ya kuhitimu  pale serikali ilipotangaza kuwa kuanzia mwakani luga itakayotumika kufundishia itakuwa ni kiswahili badala ya kiingereza tangu shule za awali hadi vyuo vikuu hapa nchini Wakiongea na na Blog hii, Shani Shaba mwanafunzi tutuba sekondari Emmanuel Gwegenyeza mtau wa elimu Sharehe Makunga mkuu shule ya Tutuba sekondari kwa nyakati tofauti wanafunzi hao ambao ni Shani Shabani,Balosha Josephati  wa shule ya sekondari Tutuba na Georg Gwamagobe wa shule ya Gwegenyeza wamesema kuwa luga iliyozoeleka  na kutumika vizuri katika ngazi zote za elimu ni kiingereza  mara itakapobadirika gafra uende wengi wakashindwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao nakuongeza kuwa kama watakuwa wanafahamu kiswahili tu w...

Uchaguzi wa ubunge ambao umesubiriwa kwa muda mrefu nchini Misri unaanza huku watu wakipiga kura katika balozi tofauti kote duniani.

Picha
Uchaguzi wa ubunge ambao umesubiriwa kwa muda mrefu nchini Misri unaanza huku watu wakipiga kura katika balozi tofauti kote duniani. Vituo vya kupigia kura nchini Misri vitafunguliwa siku ya jumatatu. Kundi la Muslim Brotherhood lililoshinda uchaguzi wa ubunge miaka mitatu iliyopita kabla ya kupigwa marufuku halitashiriki uchaguzi huo. Bunge jipya linatarajiwa kuwa na wabunge wengi wafuasi wa aliyekuwa mkuu wa majeshi Abdul Fattah al sisi ambaye alichukua madaraka mwaka 2013 na kuchaguliwa kuwa rais mwezi Mei mwaka uliopita.

Israel:Mpalestina aliyewashambulia polisi auawa

Picha
Polisi wa Israeli wanasema kuwa wamemuua kwa kumpiga risasi mwanamume Mpalestina mjini Jerusalem baada ya kujaribu kuwashambulia. Msemaji wa polisi anasema kuwa polisi walimkaribia mwanamume huyo kabla ya kumdunga kisu. Hii ni kati ya misururu ya visa sawa na hivyo ambapo zaidi ya watu 40 wameuawa. Waziri wa mashauri ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewapigia simu waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu pamoja na rais wa Palestina Mahmoud Abbas na kuwataka kuleta utulivu.

Maelfu ya Watu wamekusanyika mjini Ankara nchini Uturuki kuomboleza kwa ajili ya Watu takriban 95 waliouawa kwa milipuko miwili ya mabomu.

Picha
Maelfu ya Watu wamekusanyika mjini Ankara nchini Uturuki kuomboleza kwa ajili ya Watu takriban 95 waliouawa kwa milipuko miwili ya mabomu. Watu wanaounga mkono Chama cha Kikurdi ambao walikuwepo kwenye mkutano katika eneo ambalo mabomu yalilipuka wanaamini kuwa idadi ya kweli ya waliopoteza maisha ni Watu 128. Waombolezaji nchini Uturuki wakati wa mazishi Vyanzo vya ulinzi vinasema kuwa vinashuku kundi la wanamgambo wa IS kuhusika kwenye shambulio hilo. Serikali imekana vikali madai kuwa imehusika katika mashambulizi hayo. Milipuko ya mabomu ilitokea karibu na kituo cha treni cha mjini Ankara wakati watu walipokusanyika kwa ajili ya matembezi yaliyoandaliwa na makundi ya mrengo wa kushoto yakishinikiza kukoma kwa mapigano kati ya Serikali ya Uturuki na wanamgambo wa kikurdi. Katika hali iliyotarajiwa, wanamgambo wa PKK walitangaza kuweka silaha chini siku ya jumamosi, wakitoa wito kwa wapiganaji wake kuachana na mapigano ya msituni nchini Uturuki , isipokuwa ikiwa ni kwa...

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametetea uamuzi wa nchi yake wa kuchukua hatua za kijeshi nchini Syria, na kusema lengo ni “kusaidia utawala halali” wa Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Picha
Urusi ilianza mashambulio ya kutoka angani Syria Septemba 30 Putin amesema magaidi wakiteka Syria wanaweza kuwa tishio kwa Urusi Rais wa Urusi Vladimir Putin ametetea uamuzi wa nchi yake wa kuchukua hatua za kijeshi nchini Syria, na kusema lengo ni “kusaidia utawala halali” wa Rais wa Syria Bashar al-Assad. Bw Putin aliambia runinga ya taifa ya Urusi kwamba Moscow pia inataka kuunda mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa maafikiano ya kisiasa. Alikanusha madai kwamba mashambulio ya ngani ya Urusi yanalenga makundi ya upinzani badala ya wapiganaji wa Islamic State. Wanajeshi wa Syria wamepiga hatua kubwa dhidi ya waasi wanaopinga serikali. Wanajeshi wa Assad walipata mafanikio makubwa mikoa ya Idlib, Hama na Latakia, habari zilizothibitishwa Jumapili na maafisa mjini Damascus na pia wanaharakati wa upinzani. Eneo kuu la vita sasa liko karibu na barabara kuu inayounganisha mji mkuu na miji mingine mikubwa, ukiwemo Aleppo, na wanajeshi wa Assad wanaaminika kulenga kufungi...

Mpalestina mja mzito auawa na jeshi la Israeli

Picha
Wizara ya afya huko Gaza inasema mwanamke mmoja Mpalestina aliyekuwa mjamzito, na mwanawe wameuawa katika shambulio lililofanywa na majeshi ya Israel huko . Maafisa hao wanasema nyumba ya mama huyo iliporomoka baada ya ndege za kijeshi za israeli kufyatua makombora katika majumba yanayoaminika kuwa handaki za wapiganaji wa Hamas. Mama huyo na mwanawe walishindwa kujinasua nyumba yao ilipoporomoka kutokana na kishindo hicho cha makombora mazito na hivyo kupoteza maisha yao . Nyumba yao inasemekana kuwa mkabala na chuo cha kijeshi cha wanamgambo wa Hamas. Ndege za kijeshi za Israeli zimeanza upya mashambulio huko Gaza huku kukiwa na wasiwasi wa hali hiyo ya makabiliano huenda ikazidi baina ya waisraeli na wa- Palestina . Israeli inadai kuwa inalenga vituo vya silaha vya Hamas baada ya roketi mbili kurushwa huko Israel siku 2 zilizopitaWaziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, amezunguzma na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu na vile vile rais wa Palestinian Mahmo...

Ili kudumisha Amani na usalama wa Raia na na ulinzi wa mali zao ni lazima watendaji waliopewa dhama katika vyombo husika kuhakikisha wanafuata maadili ya kazi zao

Picha
Major Edwin Ndangula mshauri wa mgambo wilaya ya kibondo mgeni rasmi kwa niaba ya  mkuu wa wilaya ya kibondo  Ili kudumisha Amani na usalama wa Raia na na ulinzi wa mali zao ni lazima watendaji waliopewa dhama katika vyombo husika kuhakikisha wanafuata maadili ya kazi zao Akiongea katika hafra ya kufunga mafunzo ya awali ya Jeshi la Mgambo 2015 iliyofanyika kwaenye kijiji cha Twabagondozi wilaya ya kibondo mkoa wa kigoma kaimu  mkuu wa wilaya hiyo Peter Toyma akiwakilishwa na Major Elisha Ndangula ambaye ni mshauri wa mgambo wa wilaya kibondo, amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kutojiingiza katika vitendo vya kuhatarisha amani Ameeleza kuwa wahitimu hao wamepata mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya siraha za moto hiyo ni vyema wakayatumia kwa manufaa ya Taifa huku wakizingatia viapo vyao na kutojiingiza katika ushabiki wa kiasa ikizingatiwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu Katika lisara yao wahitimu hao iliyo...

Ukosefu wa kipato cha kutosha na mmomonyoko wa maadili katika familia nyingi hapa nchini ni sababu mojawapo inayowa kupelekea watu wengi kuvunja Taratibu na sheria za nchi katika sekta mbalimbali makazini

Picha
Ukosefu wa kipato cha kutosha na mmomonyoko wa maadili katika familia nyingi hapa nchini ni sababu mojawapo inayowa kupelekea watu wengi kuvunja Taratibu na sheria za nchi katika sekta mbalimbali makazini Wakiongea na Clouds kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Kibondo Mkoani Kigoma wamsema kuwa katika sekta ya usfirishaji wa Abiria na mizigo hususa ni usafiri wa Pikipiki maalufu Bodaboda wamekuwa wakikiuka taratibu na sheria za Barabarani kama kubeba watu zaidi ya mmoja na kubeba mizigo mipana hali ambazo zimekuwa zikipekea kuwepo kwa ajali nyingi za pikipiki Hata hivyo wameeleza kuwa tatizo kubwa licha ya umasikini ni kuharibika maadili makazini hususa kwa wasimamizi wa taratibu hizo kama polisi wa usalama barabarani kutafanya kwa dhati halinayopekea madhala makubwa katika jamii Steevin Joka mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani kituo cha Polis Kibondo Jastin Isaka mwendesha pikipiki Kibondo Nao baadhi waendesha Pik...

Watanzani wametakiwa kuachana na dhana potofu na kupenda jifunza ili kupata uelewa juu ya Taasisi za serikali na shughuli zake kuliko kuendelea na minong’no isiyokuwa na maana kwa kulipaka matope jeshi la kujenga Taifa kuwa nila unyanyasaji

Picha
Vijana jkt wakiwa kwenye Gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi Luten Conal Amos Gerad mkuu wa kikos 824 Kj Kanembwa Jkt Mkuu wa wilaya ya Kakonko Pete Toima mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Watanzani wametakiwa kuachana na dhana potofu na kupenda jifunza ili kupata uelewa juu ya Taasisi za serikali na shughuli zake kuliko kuendelea na minong’no isiyokuwa na maana kwa kulipaka matope jeshi la kujenga Taifa kuwa nila unyanyasaji Hayo yamewekwa wazi na Mkuu wa kikosi cha 824 kj Kanembwa Jkt Luten Colnal Amos Gerard kilichoko wilayani Kakonko mkoa wa kigoma wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vina mujibu wa sheria operation Kikwete. Ameeleza kuwa kumekuwepo na maneno kuwa Jeshi la kujenga Taifa hapa nchini katika Vikosi vyake kuwa kuna manyanyaso na mateso,  hali inayopelekea baadhi ya vija kukwepa kujiunga na jeshi hilo  maneno ambayo hayana ukweli wowote bali kulipaka m...