Israel:Mpalestina aliyewashambulia polisi auawa

Polisi wa Israeli wanasema kuwa wamemuua kwa kumpiga risasi mwanamume Mpalestina mjini Jerusalem baada ya kujaribu kuwashambulia.
Msemaji wa polisi anasema kuwa polisi walimkaribia mwanamume huyo kabla ya kumdunga kisu.
Hii ni kati ya misururu ya visa sawa na hivyo ambapo zaidi ya watu 40 wameuawa.
Waziri wa mashauri ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewapigia simu waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu pamoja na rais wa Palestina Mahmoud Abbas na kuwataka kuleta utulivu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao