Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi sekondari wilayani kibondo na Kakonko mkoa wa Kigoma wameeleza wasiwasi wao kushindwa kufanya vizuri katika masomo na kukosa ajira baada ya kuhitimu pale serikali ilipotangaza kuwa kuanzia mwakani luga itakayotumika kufundishia itakuwa ni kiswahili badala ya kiingereza tangu shule za awali hadi vyuo vikuu hapa nchini
Wanafunzi wa shule ya sekondari Tutuba wakiwa Darasani |
Wakiongea na na Blog hii,
Shani Shaba mwanafunzi tutuba sekondari |
Emmanuel Gwegenyeza mtau wa elimu |
Sharehe Makunga mkuu shule ya Tutuba sekondari |
Lugha ni chombo muhimu sana cha mawasiliano kilichoundwa na sauti zanasibu za kusemwa na kutumiwa na jamii ya utamaduni fulani. Jinsi ambavyozipo jamii nyingi za tamaduni mbalimbali duniani, vivyo hivyo ziko lughambalimbali zilizoundwa kukidhi haja ya mawasiliano ya tamaduni mbalimbali.
Maingiliano ya jamii zenye tamaduni na lugha mbalimbali yanayotokana namashirikiano katika shughuli za biashara na nyinginezo za kijamii, huzusha hajaya kuwepo kwa lugha moja itakayoweza kuwaungaanisha watu hao wenye tamaduni na lugha mbalimbali.
Hata hivyo wengine wamekuwa tofauti na wezao kwa kudai kuwa Luga ya kiswahili ni ya asili katika nchi hii na utaratibu huo unaweza kumfanya mwanafunzi kumuelewa mwalimu ipasavyo
Nao walimu wamekuwa na yao yakueleza kwamba muda ni mfupi sana kuanza kutekeleza hazima kwani inaweza kuchukua muda murefu kubadilisha mitaala hasa katika luga hivyo uenda zoezi hilo likakwama kuzaa matunda kama alivyosema Sarehe Makunga mwalimu toka shule ya sekondari Tutuba
Kuna faida na hasara katika kutumia luga ya kiswahili kufundishia kwani luga hiyo inatumika kwa watanzania wote ni asili ya taifa hili na hata mataifa mengine yanaweza kutafuta watu toka Tanzaniaili wakafundishe kiswahili kwenye nchi zaoalisema Emmanuel Jeremia mkurugenzi wa Shule ya sekondari Gwegenyeza huku mmoja wa wakazi wa kibondo Agnes Katoto akieleza kuwa ni vema utaratibu uendelee kama ilivyo kuwa awali
Na kuongeza kuwa nyakati za hivi karibu elimu katika nchi hii ilishuka kiwango chake kwa wanafunzi kufanya vibaya huku kukiwepo sababu mbalimbali lakini kinachoonekana ni kubadilika kwa mitaala kila wakati hatua inayooneka kuwachanganya wanafunzi.
Joseph Tirutangwa Afisa elimu shule za msingi wilaya ya kibondo yeye amewatoa wasiwasi wananfuzi hao kuwa utakuwepo utaratibu kuhakikisha watu wanafahamu kiingereza na wala tamko hilo la serikali halijasema kuwa luga hiyo haitatumika mashuleni tatizo ni kwamba hata walimu wa sasa hawana mbinu nzuri za kufundisha kiingereza
Aidha Tirutangwa alisema kuwa zipo baadhi ya nchi nyingi dunia zinazotumia Luga zao za asili katika mambo yote ikiwa ni pamoja na kufundishia mashuleni na shuguli zao zinaenda vizuri
Maoni
Chapisha Maoni