Ili kudumisha Amani na usalama wa Raia na na ulinzi wa mali zao ni lazima watendaji waliopewa dhama katika vyombo husika kuhakikisha wanafuata maadili ya kazi zao






Major Edwin Ndangula mshauri wa mgambo wilaya ya kibondo mgeni rasmi kwa niaba ya  mkuu wa wilaya ya kibondo 






Ili kudumisha Amani na usalama wa Raia na na ulinzi wa mali zao ni lazima watendaji waliopewa dhama katika vyombo husika kuhakikisha wanafuata maadili ya kazi zao

Akiongea katika hafra ya kufunga mafunzo ya awali ya Jeshi la Mgambo 2015 iliyofanyika kwaenye kijiji cha Twabagondozi wilaya ya kibondo mkoa wa kigoma kaimu  mkuu wa wilaya hiyo Peter Toyma akiwakilishwa na Major Elisha Ndangula ambaye ni mshauri wa mgambo wa wilaya kibondo, amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kutojiingiza katika vitendo vya kuhatarisha amani

Ameeleza kuwa wahitimu hao wamepata mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya siraha za moto hiyo ni vyema wakayatumia kwa manufaa ya Taifa huku wakizingatia viapo vyao na kutojiingiza katika ushabiki wa kiasa ikizingatiwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu


Katika lisara yao wahitimu hao iliyosomwa na Bw Dickson Kabandumba wameiomba serikali kupitia jeshi la wananchi Tanzania JWTZ kutoa mafunzo ya juu kwa wananmgambo ili kuongeza weledi katika maswala ya ulinzi na kuwaondolea changamoto ya upatikanaji wa vitambulisho vya kudumu na sale  za jeshi hilo hali ambayo imekuwa ikiwasababishia vikwa vya upatikanajia wa ajira katika taasisi za ulinzi

Hata hivyo baadhi yao wameongeza kuwa mafunzo waliyoyapata watayatumia kwa uaminifu kulingana taratibu watakazopewa na kuuomba uongozi kutowasahau mara wanapo tawanyika kwenda katika maeneo ya kazi bali ushirikiano uwepo na kuwapa vipaumbele katika maswala ya ajira


Wahitimu hao waliomaliza na kutunukiwa vyeti wamemaliza mafunzo hayo wakiwa idadi yao 68 huku wengine 30 wakitoroka tangu walipoanza juni 1 mwaka huu ambapo walikuwa 98
Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao