Mpalestina mja mzito auawa na jeshi la Israeli

Wizara ya afya huko Gaza inasema mwanamke mmoja Mpalestina aliyekuwa mjamzito, na mwanawe wameuawa katika shambulio lililofanywa na majeshi ya Israel huko .
Maafisa hao wanasema nyumba ya mama huyo iliporomoka baada ya ndege za kijeshi za israeli kufyatua makombora katika majumba yanayoaminika kuwa handaki za wapiganaji wa Hamas.
Mama huyo na mwanawe walishindwa kujinasua nyumba yao ilipoporomoka kutokana na kishindo hicho cha makombora mazito na hivyo kupoteza maisha yao
.Nyumba yao inasemekana kuwa mkabala na chuo cha kijeshi cha wanamgambo wa Hamas.
Ndege za kijeshi za Israeli zimeanza upya mashambulio huko Gaza huku kukiwa na wasiwasi wa hali hiyo ya makabiliano huenda ikazidi baina ya waisraeli na wa- Palestina .
Israeli inadai kuwa inalenga vituo vya silaha vya Hamas baada ya roketi mbili kurushwa huko Israel siku 2 zilizopitaWaziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, amezunguzma na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu na vile vile rais wa Palestinian Mahmoud Abbas kujaribu kuidhibiti hali hiyo
.Habari hii ni kwa mujibu wa BBC.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji