Jamii wilayani Kibondo imetakiwa kufuata taratibu za usafi kwa kutokuuza na kula, kiholela vyakula kama mbogamboga na matunda yaliyomenywa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu
Mwemezi Muhingo Kibondo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Bi. Ruth Msafiri, amepiga marufuku watumishi wa serikali Wilayani humo kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo amesema linaweza kukwamisha ufanisi katika shughuli za umma Wilayani Kibondo. Bi. Msafiri aliyasema hayo jana katika kikao kilichowahusisha watumishi wa idara ya afya wilayani kibondo, wakiwemo viongozi kutoka taasisi mbalimbali wilayani humo, lengo ikiwa ni kujadili namna ya kuweka tahadhari ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu, endapo utajitokeza wilayani humo. Aidha alieleza kuwa kila mtumishi wa serikali anapaswa kuwajibika kikamilifu katika nafasi yake, ili kuhakikisha kuwa dalili za ugonjwa huo zinakomeshwa kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zoezi la usafi wa mazingira wilayani humo linafanyika kila siku za aihamisi, kwa kushirikisha watumishi wote wa serikali pamoja na wananchi. Hata hivyo amekemea vitendo vya baadhi ya watumishi wa serikali kuamua kujipa ma...