Marekani imeitaka serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya raia wa Zanzibar katika uchaguzi wa urais uliopita.
Akimtumia risala za pongezi rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa ushindi wake wa uchaguzi mkuu uliopita, waziri wa maswala ya kigeni nchini humo John Kerry amesema kuwa Marekani inaendelea kukerwa na hatua ya kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo.
''Tunautaka utawala mpya kuhakikisha kuwa maamuzi ya raia wa Zanzibar yanazingatiwa naHii ni mara ya pili kwa Marekani kuzungumzia hatua ya ZEC kufuta matokeo hayo.
Amesisitiza wito wa Marekani wa kutofutiliwa mbali kwa matokeo hayo huku akizitaka pande zote kushirikiana kwa lengo la kufanikisha mchakato huo wa kidemokrasia kwa uwazi na amani.
Rais Magufuli |
Maoni
Chapisha Maoni