Watu wenye silaha wamewapiga risasi na kuwauwa watu saba usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu wa Burundi- Bujumbura

Watu hao waliokuwa katika kilabu cha burudani mjini Bujumbura waliamrishwa walale chini kabla ya kufyatuliwa risasi na kuuawa papo hapo.
Meya wa mji huo ametaja kisa hicho kama mauwaji ya
kinyama.
 7 na kuwajeruhi wengine wawili alisema Freddy Mbonimpa meya wa mji huo.Mauaji hayo yanatukia katika siku ya mwisho iliyotolewa na serikali kwa raia walioko na silaha kuzisalimisha kwa vyombo vya dola.
Awali Serikali ilikuwa imewapa watu fursa ya kusalimisha silaha walizo nazo lau sivyo polisi wachukue hatua kali dhidi yao kuwapokonya.
Hapo jana wenyeji wa vitongoji vya mji wa Bujumbura walionekana wakitoroka makwao kwa hofu ya makabiliano na vyombo vya serikali.
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura, aliwaona watu wamebeba magodoro na kadhalika katika mabarabara, wakihamia kwenda kwa marafiki na jamaa katika mitaa salama.Watu zaidi ya laki mbili wamekimbilia nchi za nje.
Katika juma lilopita pekee , watu 13 wamekufa, hasa kwenye mitaa ambako upinzani una nguvu.
Idadi ya watu waliouawa sasa imegonga 20 na kuongeza idadi ya awali ya watu 200 ambao wameuwawa katika wimbi la machafuko ya kisiasa nchini humo, tangu mwezi Aprili, pale rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia ya kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu.
Awali wenyeji wa vitongoji vya mji wa Bujumbura walionekana wakitoroka makwao kwa hofu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji