Watu wengi wanakimbia baadhi ya mitaa ya Bujumbura, Burundi, kabla ya muda uliowekwa na serikali wa leo usiku, ambapo watu wenye silaha wanatakiwa kusalimisha silaha zao.
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura, aliona watu wamebeba magodoro na kadhalika katika barabara, wakihamia kwa marafiki na jamaa katika mitaa salama.
Umoja wa Mataifa unasema, watu karibu mia mbili wameuwawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili, katika fujo zilizochochewa na tangazo la Rais Pierre Nkurunziza kusema anagombea muhula wa tatu wa uongozi.
Watu zaidi ya laki mbili wamekimbilia nchi za nje.
Katika juma lilopita peke yake, watu 13 wamekufa, hasa kwenye mitaa ambako upinzani una nguvu.
Raia waendelea kuitoroka mitaa ya mji wa Bujumbura |
Maoni
Chapisha Maoni