Ukakamavu ni jambo la muhimu sana katika maisha ya Binadamu kwani uujenga na kuuweka sawa mwili

Hao ni baadhi ya vijana wakiwa kwenye Gwaride la kuhitimu  katika moja ya mafunzo ya awali ya kijeshi katika kikosi cha 824 kj Kanembwa Jkt kilicho wilayani Kakonko moani Kigoma

Mafunzo hayo yalifungwa rasmi na Mkuu wa mkoa wa Kigoma Bw, Issa Machibya, kwa kuwakilishwa na mkuu wa wilaya kakonko Peter Toyma na kuwapandisha kutoka daraja la clut na kuwa service Girls na Boys huku jumbe mbalimbali zikitolewa kwa ajili ya kuwaasa kufuata taratibu za nchi na kutimiza viapo vyao

Vijana hao ni kwa mujibu wa sheria, hususa ni wale waliomaliza  kidato cha sita 2015 katika shule mbalimbali za sekondari hapa nchini  na kundi hilo kupewa jina la Oparation Kikwete

Mkuu wa Kikosi hicho Luten Conal Amos Gerad na viongozi wengozi wengine wakiwemo maafisa wa jeshi hilo walitoa jumbe mbalimbali kwa jamii ya  kitanzania juu ya kulifahamu na kuthamini kazi zake kwani lipo kwa mujibu sheria za nchi na ni kwa ajili ya watanzania wote, huku vijana wenyewe wakitoa shukrani zao wa wazazi na serikali kwa kuwapa fulsa ya kujiunga na jeshi hilo




         
Peter Toyma dc Kakonko mgeni rasmi wa niaba ya Rc Kigoma

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji