Jamii wilayani Kibondo imetakiwa kufuata taratibu za usafi kwa kutokuuza na kula, kiholela vyakula kama mbogamboga na matunda yaliyomenywa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu

Mwemezi Muhingo Kibondo

Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Bi. Ruth Msafiri, amepiga marufuku watumishi wa serikali Wilayani humo kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo amesema linaweza kukwamisha ufanisi katika shughuli za umma Wilayani Kibondo.

Bi. Msafiri aliyasema hayo jana katika kikao kilichowahusisha   watumishi wa idara ya afya wilayani kibondo, wakiwemo viongozi kutoka taasisi mbalimbali wilayani humo, lengo ikiwa ni kujadili namna ya kuweka tahadhari ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu, endapo utajitokeza wilayani humo.


Aidha alieleza kuwa kila mtumishi wa serikali anapaswa kuwajibika kikamilifu katika nafasi yake, ili  kuhakikisha kuwa dalili za ugonjwa huo zinakomeshwa kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zoezi la usafi wa mazingira wilayani humo linafanyika kila siku za aihamisi, kwa kushirikisha watumishi wote wa serikali pamoja na wananchi.

Hata hivyo amekemea vitendo vya baadhi ya watumishi wa serikali kuamua kujipa mapumziko yasiyokuwa rasmi wakatiti siku za kujumuika katika zoezi la usafi na kuwataka wakuu wote wa idara kuangalia mahudurio sehemu za kufanyia usafi na ambaye hatakuweo ifahamike kuwa hakufika kazini 


Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya ya Kibondo Bw. Ramadhani Mrangi amesema idara ya afya wilayani kibondo imekwisha kuandaa timu ya wataalamu wa afya watakao kuwa tayari kuhudumia wagonjwa wa kipindupindu ambapo pia amewataka wananchi kuzingatia usafi hasa katika maandalizi ya vyakula.

Katibu wa ccm wilaya ya kibondo Hamisi Kananda ambaye alialikwa kushiriki kwenye kikao hicho amesema kuwa hali ya usafi ni mbaya sana mitaani tofauti na repoti za idara ya afya kuwa usafi umeimalika huku Kassm Seif shehe wa wilaya hiyo akilalamikia uchafu unazolewa na idara hiyo na kwenda kuutupa katika maeneo ya makazi ya watu hatua ambayo ni hatari kwa afya za watu

Kampeni ya usafi wa mazingira ilipangwa kuendelewa kwa kushirikiana kati ya wananchi na watumishi wa serikali kufanya usafi kwa pamoja siku alhamisi utaratibu ambao ulishindikana kuendelezwa kama wilaya zingine zinavyofanya na uenda ndiyo kuwepo hali uchafu na kuleta migongano 


Hatua hiyo imefikiwa baada ya wananchi kuanza kupigia kelele mrundikano wa taka katika vizimba vilivyoko katika mji wa kibondo na kukaa muda murefu bila kuzolewa hali inayoashiria kutokea magonjwa ya mripuko kama kipindupindu, ugonjwa ambao umeshayakumba baadhi ya maeneo nchini

-- 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao