Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2015

Wastaafu wa kada mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa chachu ya maenedeleo kwa kuwasadia wale walioko makazini kwa kutoa ushauri juu ya vikwazo walivyo kutana navyo kazini ikiwamo, na mafanikio kwa ujumlana namna ya kufanya kazi kwa welediNdyaki Majo katibu cwt Kibondo

Picha
Wastaafu wa kada mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa chachu ya maenedeleo kwa kuwasadia wale walioko makazini kwa kutoa ushauri juu ya vikwazo walivyo kutana navyo kazini ikiwamo, na mafanikio kwa ujumlana namna ya kufanya kazi kwa weledi Wito huwo  umetolewa na Katibu wa chama cha walimu wilaya kibondo Bw,Ndyaki Majo wakati wa hafra fupi ya kuwaaga walimu wastaafu iliyofanyika kwenye ukumbi wa chama hicho mjini kibondo. Majo amesema kuwa hivi sasa taaluma ya ualimu imejumuisha vijana  wengi ambao wanapangiwa kufanya kazi katika maeneo mengi ambao wanahitaji maelekezo waweze kupata ufanisi katika utendaji kazi hivyo, kama ni kustaafu ni kwa mujibu wa taratibu tu  lakini mchango wao bado unahitajika Nae mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya kibondo Tilimio Nzigo, amesema kuwa lengo la kutoa mkono wa kwaheri kwa wastaafu, ni kutambua  mchango wao walioutoa kwa umma, na kuongeza kuwa chama kinatambua kuwapo kwa changamoto zinazoendelea kuwakabili w...

Wadau wa maendeleo ya jamii na mashirika mbalimbali na serikali kwa ujumla wametakiwa kuyaangalia kwa jicho la huruma makundi ya walemavu waishio vijijini kwani baadhi mahitaji yao ni makubwa kulingana na viwango vya ulemavu

Picha
Muhingo Mwemezi Kakonko Wadau wa maendeleo ya jamii na mashirika  mbalimbali na serikali kwa ujumla wametakiwa kuyaangalia kwa jicho la huruma makundi ya walemavu waishio vijijini kwani baadhi mahitaji yao ni makubwa kulingana na viwango vya ulemavu Akiongea katika Kijiji cha Malenga wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Mbunge wa jimbo la Buyungu Kasuku Bilago amesema kuwa jamii zinaishi vijijini hazina uwezo wa kuwasidia ipasavyo walemavu ikilinganishwa na vipato vyao kiuchumi hatua inayopelekea wengi wao kukata tamaa  Hata hivyo Bilago alitoa msahada wa baiskeli nne zenye Magurudumu manne, zenye thamani ya tsh milion mbili kwa baadhi ya walemavu wa miguu wanaotembea kwa kujivuta ili ziweze kuwasaidia kwenda sehemu moja hadi nyingine na kuiomba serikali kuelekeza nguvu zake kwa makundi hayo yanayoishi vijijini  Baadhi ya  walionufaika na msahada huo ambao ni Chubwa Maasbo Mkazi wa malenga na Erasmus Bilunda mkazi Kasuga wameeleza changamoto walizokuwa w...

Wakazi wa Kijiji cha Kikulazo Kata ya Lugenge, wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameiomba serikali kulishawishi shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa matifa UNHCR kujenga kituo maalum cha kuwapokelea wakimbizi toka nchini Burundi wanaoendelea kukimbia machafuko ya kisiasa nchini mwao, ili kunusulu afya za wanakijiji wanaishishi mipakani baada ya raia hao kuanza kukimbia na kukosa sehemu maalum ya kufikia hatimae kuchafua mazingira

Picha
Wakazi wa Kijiji cha Kikulazo Kata ya Lugenge, wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameiomba serikali kulishawishi shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa matifa UNHCR kujenga kituo maalum cha kuwapokelea wakimbizi toka nchini Burundi wanaoendelea kukimbia machafuko ya kisiasa nchini mwao, ili kunusulu afya za wanakijiji wanaishishi mipakani baada ya raia hao kuanza kukimbia na kukosa sehemu maalum ya kufikia hatimae kuchafua mazingira Waliliiambia gazeti hili kijijini hapo,jana kuwa hivi sasa hali ni mbaya katika kijiji hicho kwani kimekuwa kikipokea wakimbizi wengi wanaokingia Tanzania kwa ajili ya kuomba hifadhi na kwakuwa hakuna eneo maalum la kuwapokelea lilitengwa, ufikishiwa katika gala la la kutunzia vyakula  hali ina inayopelekea kjisadia hovyo, pia na huduma za kijamii hazipo Beatus Mpera, ambae ni mkazi wa kijiji hicho ameleza kuwa hofu yao kubwa ni kutokea magonjwa ya mlipuko na mengineyo katika maeneo hayo na kuongeza kuwa huduma za muhimu kama ameneo ...

Miili zaidi ya 34 imepatikana katika barabara za mji mkuu wa Burundi huku machafuko yakiendelea, huku jeshi likisema watu 87 waliuawa Ijumaa. Mwandishi wa BBC ameona maiti 21 katika mtaa mmoja wa Bujumbura na maafisa wa serikali wamesema kuna miili mingine 13.

Picha
Miili zaidi ya 34 imepatikana katika barabara za mji mkuu wa Burundi huku machafuko yakiendelea, huku jeshi likisema watu 87 waliuawa Ijumaa. Mwandishi wa BBC ameona maiti 21 katika mtaa mmoja wa Bujumbura na maafisa wa serikali wamesema kuna miili mingine 13. Maiti nyingi zinaonekana kuwa za vijana waliouawa kwa kupigwa risasi, baadhi wakiwa wamefungwa mikono yao ikiwa pamoja mgongoni. Miili hiyo imepatikana siku moja baada ya watu wenye silaha kushambulia maeneo matatu ya jeshi. Jeshi la Burundi limesema watu 87 waliuawa kwenye mapigano ya Ijumaa, wanane kati yao wakiwa maafisa wa usalama. Machafuko yameendelea kutatiza Burundi tangu kutibuliwa kwa jaribio la kupindua serikali mwezi Mei na maandamano yaliyofanyika kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa mara nyingine, wazo alilotangaza Aprili. Bw Nkurunziza alishinda uchaguzi uliofanyika Julai.

Viongozi wanaoaminiwa na kupewa dhamana ya kuwaongoza wananchi wametakiwa kujijengea mazingira ya uaminifu kwa kutenda yale yanayostaili na kuenenda kwa kufuata sheria taratibu na kutimiza viapo vyao ili kuondoa kukata tamaa kwa wananchi wao

Picha
Viongozi wanaoaminiwa na kupewa dhamana ya kuwaongoza wananchi wametakiwa  kujijengea mazingira ya uaminifu kwa kutenda yale yanayostaili na kuenenda kwa kufuata sheria  taratibu na kutimiza viapo vyao ili kuondoa kukata tamaa kwa wananchi wao Erick Marey Hakimu wa wilaya ya Kibondo wakati wa kuwahapisha madiwani Halmashauri ya Kakonko Peter Toyima Dc Kakonko Akizungumza juzi, katika uzinzinduzi wa Baraza la Halmashauri la walaya ya Kakonko Mkoani Kigoma,  Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Kibondo Erick Marey wakati wa kuwahapisha madiwani alisema kuwa kiapo ni ishara ya utii kwa mlengwa hivo ni lazaima kifuatwe kwa kuyatenda yale kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na kinyume na hasipofuata taratibu hizo anastaili kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuwajibishwa Katika kikao hicho mara baada ya kuhapishwa madiwani hao, ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti  wa halmashauri na makamu wake ambapo Juma Maganga kata ya kakonko, alipata kura 12 ...

Wakulima na wafugaji wakijiji cha Gwanumpu Kata ya Gwanumpu wilayani kakonko mkoani kigoma wameitaka serikali kuingilia katimgogoro uliopo kati ya wafugaji na wakulima hali ambayo huwafanya kulipiziana visasi kilawakati

Picha
Wakulima na wafugaji wakijiji cha Gwanumpu Kata ya Gwanumpu wilayani kakonko mkoani kigoma wameitaka serikali kuingilia katimgogoro uliopo kati ya wafugaji na wakulima hali ambayo huwafanya kulipiziana visasi kilawakati. Mtondo Mtondo mkulima wa Kijiji cha Gwanumpu Bw, Toyi Slivester Diwani kata ya Gwanumpu -Wakiongea katika mkutano wa hadhara jana uliofanyika kijiji hapo, wamesema kwasasa wakulima na wafugaji hawaelewani kwa kile wanachokidai kuwa kila mmoja huona yuko sahihi katika eneo  ambalo linadaiwa kutengwa kwa ajili ya malisho na uonekana kuwa na rutuba nzuri pamoja na nyasi nzuri za kulishia mifugo. Bw.Godwini George ni mmoja wa wafugaji anasema eneo hilo awali lilitengwa kwa ajili ya wafugaji lakini kwasasa wakulima wamevamia maeneo hayo huku Bw.Mtondo Danieli ambae ni mkulima akidai kuwa amefanya shughuli za kilimo katika maeneo hayo kwa muda miaka sabana hakuna aliyewahi kumueleza kuwa eneo hilo ni kwa ajili ya malisho ya mifungo Aidha...