Viongozi wanaoaminiwa na kupewa dhamana ya kuwaongoza wananchi wametakiwa kujijengea mazingira ya uaminifu kwa kutenda yale yanayostaili na kuenenda kwa kufuata sheria taratibu na kutimiza viapo vyao ili kuondoa kukata tamaa kwa wananchi wao
Viongozi wanaoaminiwa na kupewa dhamana ya kuwaongoza wananchi wametakiwa kujijengea mazingira ya uaminifu kwa kutenda yale yanayostaili na kuenenda kwa kufuata sheria taratibu na kutimiza viapo vyao ili kuondoa kukata tamaa kwa wananchi wao
Erick Marey Hakimu wa wilaya ya Kibondo wakati wa kuwahapisha madiwani Halmashauri ya Kakonko |
Akizungumza juzi, katika uzinzinduzi wa Baraza la Halmashauri la walaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Kibondo Erick Marey wakati wa kuwahapisha madiwani alisema kuwa kiapo ni ishara ya utii kwa mlengwa hivo ni lazaima kifuatwe kwa kuyatenda yale kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na kinyume na hasipofuata taratibu hizo anastaili kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuwajibishwa
Katika kikao hicho mara baada ya kuhapishwa madiwani hao, ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri na makamu wake ambapo Juma Maganga kata ya kakonko, alipata kura 12 huku mpizani wake Eliya Kanjero kata ya Gwarama, Chadema akiibuka na kura 10 kati ya 22 zilizopigwa, hivyo Juma Maganga kutangazwa mshindi na kisha kuomba ushirikiano na wananchi katika utendaji kazi
Maganga aliwataka madiwani wenzake kuahakikisha wanaondoa itikadi zao za kisiasa na kushirikiana kwa kufanya kazi na kudai kuwa hatakuwa tayari kuona migawanyiko kati yao inaendelea na watakiwa kushirikiana na si kuharibiana kazi maana kauli mbiu ya serikali ya sasa ni kuwajibika
Kwa upande wa nafasi ya makamu mwenyekiti Bw, Toyi Slivester wa kata ya Gwanumpu, ccm alipata kura 12 dhidi ya mpinzani wake Bw, Nobert Gwimo Chadema, akipata kura 10 na baadae katibu tawara wa wilaya hiyo Zainabu Mbunda, kumtangaza Toyi Slivester, kuwa mshindi wa nafasi hiyo..
Hata hivyo baadhi wakazi wa Kakonko waliohudhulia kwenye kikao hicho ambao ni Ashura Mbopewe na Angelina Baraka waliwataka viongozi hao ikiwa ni Mbunge na Madiwani kuhakikisha wanayatimiza yale waliyoyaahidi kwa wananchi wakati wa Kampeni hasa katika maeneo ya vijijini kwa wanakabiliana na changamoto nyingi kama elimu duni, Maji, Barabara ukosefu wa Pembejeo za kilimo
Kwa upande wake Peter Toyma ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo aliwataka madiwani hao kuachana na mambo yaliyopita katika kampen za uchaguzi na kushikama katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo na kusema kuwa serikali haitamvumilia yeyote atakayeenda kinyume na maelekezo
Maoni
Chapisha Maoni