Wastaafu wa kada mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa chachu ya maenedeleo kwa kuwasadia wale walioko makazini kwa kutoa ushauri juu ya vikwazo walivyo kutana navyo kazini ikiwamo, na mafanikio kwa ujumlana namna ya kufanya kazi kwa welediNdyaki Majo katibu cwt Kibondo
Wito huwo umetolewa na Katibu wa chama cha walimu wilaya kibondo Bw,Ndyaki Majo wakati wa hafra fupi ya kuwaaga walimu wastaafu iliyofanyika kwenye ukumbi wa chama hicho mjini kibondo.
Majo amesema kuwa hivi sasa taaluma ya ualimu imejumuisha vijana wengi ambao wanapangiwa kufanya kazi katika maeneo mengi ambao wanahitaji maelekezo waweze kupata ufanisi katika utendaji kazi hivyo, kama ni kustaafu ni kwa mujibu wa taratibu tu lakini mchango wao bado unahitajika
Nae mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya kibondo Tilimio Nzigo, amesema kuwa lengo la kutoa mkono wa kwaheri kwa wastaafu, ni kutambua mchango wao walioutoa kwa umma, na kuongeza kuwa chama kinatambua kuwapo kwa changamoto zinazoendelea kuwakabili walimu na kitaendelea kuishauri serikali iweze kuzitatua
Kwa upande wao baadhi ya wastaafu ambao ni Pantaleo Bilikundi na Simon Magoti waliwataka wanaoabaki makazini kufanya kazi kwa umakini wakijua kuwa taaluma ya ualimu inategemewa sana, na kujijengea tabia ya kuacha kugoma mara yanapotokea matatizo kwa kufanya hivyo ,ni kuwaadhibu wanafunzi wasiyokuwa na hatia
Walimu walioagwa kila mmoja alipewa mkono wa kwaheri kwa kupatiwa bati zenye thamani ya Tsh 320,000/ ambapo wote sita jumla ni 192,000/
Walimu wastaafu wakiwa katika moja ya kukabidhiwa zawadi cwt mjini Kibondo |
Majo Ndyaki katibu cwt Kibondo |
Pantaleo Bilikundi Mstaafu |
Baadhi ya wastaafu |
Mwenyekiti wa chama cha walimu kibondo Tilimio Nzigo, akimkabidhi zawadi mmoja wa wastaafu Simon Magoti |
Maoni
Chapisha Maoni