Wadau wa maendeleo ya jamii na mashirika mbalimbali na serikali kwa ujumla wametakiwa kuyaangalia kwa jicho la huruma makundi ya walemavu waishio vijijini kwani baadhi mahitaji yao ni makubwa kulingana na viwango vya ulemavu


Muhingo Mwemezi Kakonko

Wadau wa maendeleo ya jamii na mashirika  mbalimbali na serikali kwa ujumla wametakiwa kuyaangalia kwa jicho la huruma makundi ya walemavu waishio vijijini kwani baadhi mahitaji yao ni makubwa kulingana na viwango vya ulemavu

Akiongea katika Kijiji cha Malenga wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Mbunge wa jimbo la Buyungu Kasuku Bilago amesema kuwa jamii zinaishi vijijini hazina uwezo wa kuwasidia ipasavyo walemavu ikilinganishwa na vipato vyao kiuchumi hatua inayopelekea wengi wao kukata tamaa 

Hata hivyo Bilago alitoa msahada wa baiskeli nne zenye Magurudumu manne, zenye thamani ya tsh milion mbili kwa baadhi ya walemavu wa miguu wanaotembea kwa kujivuta ili ziweze kuwasaidia kwenda sehemu moja hadi nyingine na kuiomba serikali kuelekeza nguvu zake kwa makundi hayo yanayoishi vijijini


 Baadhi ya  walionufaika na msahada huo ambao ni Chubwa Maasbo Mkazi wa malenga na Erasmus Bilunda mkazi Kasuga wameeleza changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo katika maisha yao ya kawaidida kuwa wamekuwa wakipata taabu kwa kutembelea magoti na mikono hali ambayo ingepelea kukumbwa na magonjwa mbalimbali na kupongeza kupatiwa msahada huo.

Bw, Chubwa Masabo mlemavu akifurahia msahada wa baiskeli na Mbunge wa jimbo la Buyungu Kasuku Bilago



Wananchi waliohudhulia mkutano Mbunge Bilago

Mbunge Bilago akijaribu kusukuma Baiskeli ya mlemavu baada ya kumkabidhi ambaye ni Erasmus Bilunda

Bw, Bilunda akiendesha Baiskeli badaa ya kukabidhiwa na Mbunge



Mbunge Bilago akiongea na Mama mlemavu wa miguu


 Baadhi ya wananchi wamepongeza uamuzi wa Mbunge huyo kwa kuwatazama walemavu hao na kuwaomba wasamalia wema na wenye moyo wa kujitolea kuendelea kuwatendea wema watu wenye matatizo mbalimbali hapa nchini pasipo kusubilia serikali

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji