Wakazi wa Kijiji cha Kikulazo Kata ya Lugenge, wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameiomba serikali kulishawishi shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa matifa UNHCR kujenga kituo maalum cha kuwapokelea wakimbizi toka nchini Burundi wanaoendelea kukimbia machafuko ya kisiasa nchini mwao, ili kunusulu afya za wanakijiji wanaishishi mipakani baada ya raia hao kuanza kukimbia na kukosa sehemu maalum ya kufikia hatimae kuchafua mazingira


Wakazi wa Kijiji cha Kikulazo Kata ya Lugenge, wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameiomba serikali kulishawishi shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa matifa UNHCR kujenga kituo maalum cha kuwapokelea wakimbizi toka nchini Burundi wanaoendelea kukimbia machafuko ya kisiasa nchini mwao, ili kunusulu afya za wanakijiji wanaishishi mipakani baada ya raia hao kuanza kukimbia na kukosa sehemu maalum ya kufikia hatimae kuchafua mazingira


Waliliiambia gazeti hili kijijini hapo,jana kuwa hivi sasa hali ni mbaya katika kijiji hicho kwani kimekuwa kikipokea wakimbizi wengi wanaokingia Tanzania kwa ajili ya kuomba hifadhi na kwakuwa hakuna eneo maalum la kuwapokelea lilitengwa, ufikishiwa katika gala la la kutunzia vyakula  hali ina inayopelekea kjisadia hovyo, pia na huduma za kijamii hazipo

Beatus Mpera, ambae ni mkazi wa kijiji hicho ameleza kuwa hofu yao kubwa ni kutokea magonjwa ya mlipuko na mengineyo katika maeneo hayo na kuongeza kuwa huduma za muhimu kama ameneo ya kulala na ukosefu wa chakula hazipatikani hivyo upata shida mara shirika la kuhudumia wakimbizi linapochelewa kuwachukua kuelekea makambini.


Emmanuel Shamba mtendaji wa kijiji cha kikulazo amesema kuwa kwa siku anapokea wakimbizi 10 hadi 50, na kuwa idadi hiyo ni kubwa na wengi wanakimbia bila kuwa na kitu chochote cha kujikimu ulazimika kula maembe na wakiyakosa ulala au kushinda njaa hadi shirika la UNHCR linapofika kuwachukuwa 

Shamba aliongeza kuwa kwa hivi sasa waliopo ni 48 na ofisi yake kushirikiana na wananchi wamekuwa wakitoa misahada hasa ya chakula kwa waanga hao kwa watoto wadogo na wanawake wajawazito wakiwemo wazee wenye umri mkubwa wanaoonekana kuteseka zaidi  

Nae Kasuku Bilago ambae ni Mbunge wa jimbo la MBuyungu alisema kuwa swala hilo atalifikisha katika mamlaka husika ili liweze kutatuliwa kwa wakimbizi wawe na kituo maalum cha kuwapokelea na huduma za kibinadamu ziwepo na kuwanusulu wananchi ambao ni wenyeji wasikumbwe na magonjwa ya mlipuko kutokana hali ya usfi kulegelega


Kwa upande wao baadhi ya wakimbizi hao ambao ni Alphonce Nilagila ambae ni mwanafunzi wa sekondari na Eliza bert Mkashema, amesema kuwa amejitahidi kuvumilia baada ya wazazi wake wote kukimbia na ndugu zake kuuawa lakini ameshindwa na kuamua kuacha masomo na kukimbia baada ya vulugu kuwa kubwa

Juhudi za kumtafuta Mkuu wa wilaya hiyo Peter Toyma ili kuelezea jukum la nani anayetakiwa kujenga kituo hicho cha kupokelea wakimbizi na kama kuna ushawishi umeshafanyika ili UNCHCR wajenge kituo hicho kwa kuwanusuru wenyeji katika kijiji hicho simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani, zilishindikana..

Wakimbizi hao toka nchini Burundi wanakimbia machafuko ya kisiasa baada ya Rais wa nchiyo Peter Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu.
Wakimbizi wa Burundi wakisubiri kuandikishwa baada ya kuingia nchini Tanzania wakikimbia machafuko
Elizabeth Mkashema mkimbizi


Alphonce Nilagila Mkimbizi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji