Miili zaidi ya 34 imepatikana katika barabara za mji mkuu wa Burundi huku machafuko yakiendelea, huku jeshi likisema watu 87 waliuawa Ijumaa. Mwandishi wa BBC ameona maiti 21 katika mtaa mmoja wa Bujumbura na maafisa wa serikali wamesema kuna miili mingine 13.
Miili zaidi ya 34 imepatikana katika
barabara za mji mkuu wa Burundi huku machafuko yakiendelea, huku jeshi
likisema watu 87 waliuawa Ijumaa.
Mwandishi wa BBC ameona maiti 21 katika mtaa mmoja wa Bujumbura na maafisa wa serikali wamesema kuna miili mingine 13.Maiti nyingi zinaonekana kuwa za vijana waliouawa kwa kupigwa risasi, baadhi wakiwa wamefungwa mikono yao ikiwa pamoja mgongoni.
Miili hiyo imepatikana siku moja baada ya watu wenye silaha kushambulia maeneo matatu ya jeshi.
Jeshi la Burundi limesema watu 87 waliuawa kwenye mapigano ya Ijumaa, wanane kati yao wakiwa maafisa wa usalama.
Machafuko yameendelea kutatiza Burundi tangu kutibuliwa kwa jaribio la kupindua serikali mwezi Mei na maandamano yaliyofanyika kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa mara nyingine, wazo alilotangaza Aprili.
Bw Nkurunziza alishinda uchaguzi uliofanyika Julai.
Maoni
Chapisha Maoni