Wakulima na wafugaji wakijiji cha Gwanumpu Kata ya Gwanumpu wilayani kakonko mkoani kigoma wameitaka serikali kuingilia katimgogoro uliopo kati ya wafugaji na wakulima hali ambayo huwafanya kulipiziana visasi kilawakati

Wakulima na wafugaji wakijiji cha Gwanumpu Kata ya Gwanumpu wilayani kakonko mkoani kigoma wameitaka serikali kuingilia katimgogoro uliopo kati ya wafugaji na wakulima hali ambayo huwafanya kulipiziana visasi kilawakati.

Mtondo Mtondo mkulima wa Kijiji cha Gwanumpu

Bw, Toyi Slivester Diwani kata ya Gwanumpu


-Wakiongea katika mkutano wa hadhara jana uliofanyika kijiji hapo, wamesema kwasasa wakulima na wafugaji hawaelewani kwa kile wanachokidai kuwa kila mmoja huona yuko sahihi katika eneo  ambalo linadaiwa kutengwa kwa ajili ya malisho na uonekana kuwa na rutuba nzuri pamoja na nyasi nzuri za kulishia mifugo.

Bw.Godwini George ni mmoja wa wafugaji anasema eneo hilo awali lilitengwa kwa ajili ya wafugaji lakini kwasasa wakulima wamevamia maeneo hayo huku Bw.Mtondo Danieli ambae ni mkulima akidai kuwa amefanya shughuli za kilimo katika maeneo hayo kwa muda miaka sabana hakuna aliyewahi kumueleza kuwa eneo hilo ni kwa ajili ya malisho ya mifungo

Aidha Mtondo aliongeza kuwa wapo wafugaji ambao wamekuwa wakiharibu mazao yake mashambani na alikuwa akiwachulia hatua kwa kuwapeleka mahakamani au kwenye baraza la ardhi la kijiji hicho na wamekuwa wakimlipa fidia ila mwaka huu waliporudia tena alichukua hatua kwa kuwashitaki badala ya yake mwenyekiti wa kijiji hicho alimpa maelezo kuwa hilo ni eneo la wafugaji  

Kwa upande Mwenyekiti wa kijiji hicho Leopod Herman alisema kuwa eneo hilo ni kwa ajili ya wafugajia huku Diwaniwa kata hiyo Toyi Slivester, amesema nivema mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho kuvunja baraza la ardhi la kijiji kwa kuwa wameshindwa kutatua mgogoro huo na kuunda jingine ili kuweza kusuluhisha mgogoro huo ndani ya mwezi mmoja ili kuhepusha uvunjifu wa amani.


Hata hivyo Diwani wa kata hiyo amesema kuwa migogoro ya wakulima inaonekana kushika kasi ikiwa sababishwa tabia za  baadhi ya wafugaji kuchunga mifugo katika mashamba ya wakulima na kuwalipa garama kidogo tofauti na hasara anayoipata mkulima na kutaka usawa uwepo.

Wananchi hao waliendelea kuulamikia uongozi wa kijiji hicho pamoja na kata kwa kuwatoza michango ya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya kata ya Gwanumpu, kisha ujenzi huo kuishia njiani bila taarifa yoyote huku wajanja wachache wakidaiwa kula pesa hizo

Katika mvutano huo imegundulika kuwa kamati ya manunuzi katika ujenzi wa maabara hiyo ilinunua vifaa ambavyo havikidhi na kutaja garama kubwa ambayo si sahihi huku diwani wa kata hiyo akisisitiza kurudishwa kwa pesa hizo kiasi cha sh 2.8  milion ndani ya siku tano ikishindikana wahusika wafikishwe mahakamani kwani hali hiyo inawakatisha tama wananchi wanaojitolea

''Kuna watu wachache katika kata hii ambao walinunua vioo vya  thamani ya tsh milion 1.2 na kuandika kuwa wamenunua vifaa vya thamani ya tsh milion 2.8 sasa naagiza watu hao warudishe fedha za wananchi haraka iwezekanavyo ili wao wapange namna ya kuzifanyia kazi juu ya uendelezaji wa ujenzi wa maabara hiyo na uweze kukamilika mapema alisema Slivester diwani wa kata hiyo'' 


Bi, Magret Wangai ni mmoja watu wanaodaiwa kuhusika katika sakata la maabara kwani wakati huo alikuwa kaimu mtendaji wa kata hiyo, japo alipotakiwa kueleza ipasavyo mbele ya vyombo vya habari alidai kuwa yeye hausiki kwani swala hilo limeshapita mikononi mwa watu wengi na wengine walishahamishwa kikazi na yeye alishirika katika hatua za mwanzoni kabisa. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao