Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2016

Wadau mbalimbali wilayani kibondo mkoani kigoma wakiongozana na mkuu wa wilaya hiyo Bi.Ruthi Msafiri wametoa vitu mbalimba katika shule ya msingi nengo ya watoto wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi laki nne na nusu ili kutia hamasa kwa watoto kujisomea kwa uhuru.

Picha
Ruth Msafiri Dc Kibondo akiwa na baadhi ya watoto walemavushuleni Nengo Nashon Amosi mwalimu katika shule ya msingi Elimu maalum Nengo Kibondo Ally Kombe katibu Jumhiya ya wazazi ccm W Kibondo Wadau mbalimbali wilayani kibondo mkoani kigoma wakiongozana na mkuu wa wilaya hiyo Bi.Ruthi Msafiri  wametoa vitu mbalimba katika shule ya msingi  nengo  ya  watoto wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi laki nne na nusu ili kutia hamasa kwa watoto kujisomea kwa uhuru. Akizungumza na wazazi na walezi  katibu wa jumuia ya wazazi ccm  wilayani hapo Bw.Ally Gombe amesema hatua ya kupeleka zawadi hizo  ni baada ya kuona watoto hao wakipata adha mbalimbali wawapo shuleni na hivyo kuona umuhimu wa kuwatembelea katika njia ya kutambua haki za watoto. Amesema jamii haina budi kuwa na mazoea ya kuwatembelea watoto hao mara kwa mara ili kuweza kuwafariji pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali ambazo zitawahamasisha kusoma kwa bidii kuwafanya jisikie kuwa nao ni miongoni mwa 

Ili kuweza kuondoa kero ya umeme kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma na kuhepusha garama kubwa katika uzalishaji wa Nishati hiyo Shirika la umeme Tanesco lina mpango wa kuanzisha mradi wa kuzalisha umeme kwenye Mto Malagarasi kwa kuokoa garama kubwa za uendeshaji

Picha
Medard Kaleman Naibu waziri Nisahati Madini Ili kuweza kuondoa kero ya umeme kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma na kuhepusha garama kubwa katika uzalishaji wa Nishati hiyo Shirika la umeme Tanesco lina mpango wa kuanzisha mradi wa kuzalisha umeme kwenye Mto Malagarasi kwa kuokoa garama kubwa za uendeshaji. Sababu inayochangia garama kuwa kubwa ni mitambo ya kuzalisha umeme iliyoko katika wilaya zote za mkoa huo inatumia mafuta ambayo ununuliwa kwa kiasi kikubwa hku wateja wa umeme wakiwa ni wachache huku shirika hilo likifanya kazi kwa hasara   Akiongea na waandishi wa habari,  Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani alipokuwa wilayani  juzi Febr 20 wilayani Kibondo  wakati wa ziara ya kikazi na kutembelea miradi ya umeme mkoani humo ambapo, amesema kuwa shirika la umeme Tanesco katika Mkoa wa Kigoma linatumia shilingi million 60 kwa siku moja hatua ambayo ni hasara ikilinganishwa na idadi ndogo ya wateja wa nishati hiyo Kalemani alisema kuwa mradi wa

Walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma walipo katika mpango huo wengi wanashindwa kufika katika vituo vya ugawaji wa fedha jambo ambalo huchangia baadhi ya kaya kuzikosa fedha hizo zenye lengo la kuzisaidia kaya masikini kupata mahitaji muhimu.

Walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma walipo katika mpango huo wengi wanashindwa kufika katika vituo vya ugawaji wa fedha jambo ambalo huchangia baadhi ya kaya kuzikosa fedha hizo  zenye lengo la kuzisaidia kaya masikini kupata mahitaji muhimu. ilibainika walengwa wa mpango huo walio hama vijijini kwao na kwende kuanzisha mashamba mapya pembeni mwa Hifadhi ya Wanyama pori Moyowosi Kigosi na Vijiji vya Kumubanga na Kumuhasha wanashindwa kufika zoezi la ugawaji wa fedha kutokana na kukosa taarifa za ugawaji fedha. Jumla ya kaya 119 hazikuweza kupata fedha za uhawilishaji kwa awamu ya  tatu kutokana na uendeshaji wa shughuli za kilimo mbali na makazi ya  watu ambapo wengine 11 wamefariki dunia  hali ambayo inachangia kuwepo kwa malalamiko katika zoezi hilo. Mwenyekiti wa Kamati ya ugawaji fedha katika Kijiji cha Kisogwe kata Busunzu Bw.Yona Emmanuel Amesema Changamoto ya walengwa kuto jitokeza siku ya ugawaji wa fedha hali  hiyo imechan

Serikali imetakiwa kuhakikisha inaboresha maslahi ya walimu hapa nchini ili mpango wa elimu bure uwe na tija kwa Watanzania na elimu bora iweze kupatikana

Picha
KAKONKO       Serikali imetakiwa kuhakikisha inaboresha maslahi ya walimu hapa nchini ili mpango wa elimu bure uwe na tija kwa Watanzania na elimu bora iweze kupatikana Wakiongea jana katika uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya miaka 39 ya Chama cha mapinduzi,mmoja wa  wakazi wa kijiji cha Chulazo kata ya Nyamtukuza wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma, ambako uzinduzi huo umefanyikia  kimkoa, David Bahati,  alisema kuwa mpango wa serikali katika kuwaondolea wananchi mzigo mkubwa wa kusomesha watoto ni mzuri lakini ni vema  walimu wakaboreshewa mazingira  ili wapate moyo wa ufundishaji hasa upande wa vijijini ‘’Hivi sasa walimu wengi kulingana na mishahara midogo wameamua kuanzisha masomo ya ziada majumbani  na kutoza kiasi kikibwa cha fedha shilingi elfu kumi ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha hatua ambayo inaweza kusababisha elimu kudorola kwa sababu walimu hao uenda wasionekane katika shuguli zao za kawaida mashuleni kama jitihada za makusudi zisipo fanyika alisema Bahati’’

Mkuu wa mkoa wa kigoma kanal issa machibya amewataka vijana wanaohitimu mafunzo ya jeshi la kujenga taifa jkt kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa kuimalisha amani ya nchi pamoja na kuwabaini wahamiaji haramu ambao huingia nchini na kufanya vitendo vya uharifu.

Picha
Kakonko;  Mkuu wa mkoa wa kigoma kanal issa machibya amewataka vijana wanaohitimu mafunzo ya jeshi la kujenga taifa jkt kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa kuimalisha amani ya nchi pamoja na kuwabaini wahamiaji haramu ambao huingia nchini na kufanya vitendo vya uharifu. Kanali Machibya alitoa wito huo juzi wakati akifunga mafunzo ya awali ya jeshi la kujenga taifa jkt  kanembwa, operation Kikwete, kikosi cha 824 kj kilichopo wilayani Kakonko mkoani Kigoma, ambapo jumla ya vijana wapatao 507mujibu wa kujitolea wamehitimu mafunzo ya awali Aliongeza katika maeneo ya mipakani ndani ya mkoa wa kigoma, kumekuwa na tabia ya wahamiaji haramu kuingia nchini kupitia njia ambazo si halali, kitendo ambacho hupelekea wengi wao kuingia nchini na kutekeleza vitendo vya uharifu ikwemo uporaji. Aidha kanali machibya amewasihi vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya jeshi la kujenga taifa jkt, operation Kikwete kudumisha uzalendo na mshikamano wa taifa ili kuleta maendele

Kutokana na ujio wa Wakimbizi wanaoendelea kuingia hapa nchini wakikimbia machafuko nchini Burundi, na kuingia Tanzania Mkoani Kigoma, hali hiyo imeonekana kuihathili kiutendaji katika Hospitali ya wilaya ya kibondo Mkoani humo, kutokana na mzigo mkubwa wa wagonjwa wanaofika kupata huduma ya matibabu

Picha
Kibondo  Kutokana na ujio wa Wakimbizi wanaoendelea kuingia hapa nchini wakikimbia machafuko nchini Burundi, na kuingia Tanzania Mkoani Kigoma, hali hiyo imeonekana kuihathili kiutendaji katika  Hospitali ya wilaya ya kibondo Mkoani humo, kutokana na mzigo mkubwa  wa wagonjwa wanaofika kupata huduma ya matibabu Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Adam Jonathan aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari hospitalini hapo juzi, alipokuwa akipokea msahada wa  mashuka  stini yenye thamani ya shilingi la saba na tisin elfu yaliyotolewa na shirika la umeme nchini Tanesco kwa ajili ya wodi ya wazazi Adam aliongeza kuwa kutokana na ongezeko la watu hususa wakimbizi wanaotoka makambini hasa wajawazito wanaokuja kujifulia kwenye hospitali hiyo,  kumekuwa kukisababisha uhitaji mkubwa wa vitanda,   mashuka na Magodoro na miundo mbinu akiongeza kuwa kwa hivi sasa wanafanya upasuaji kwatu wanne hadi watano kwa siku tofauti na hapo nyuma ambapo ilikuwa zinapita siku mbili bila