Mkuu wa mkoa wa kigoma kanal issa machibya amewataka vijana wanaohitimu mafunzo ya jeshi la kujenga taifa jkt kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa kuimalisha amani ya nchi pamoja na kuwabaini wahamiaji haramu ambao huingia nchini na kufanya vitendo vya uharifu.
Kakonko; Mkuu wa mkoa wa kigoma kanal issa machibya amewataka vijana wanaohitimu mafunzo ya jeshi la kujenga taifa jkt kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa kuimalisha amani ya nchi pamoja na kuwabaini wahamiaji haramu ambao huingia nchini na kufanya vitendo vya uharifu.
Kanali Machibya alitoa wito huo juzi wakati akifunga mafunzo ya awali ya jeshi la kujenga taifa jkt kanembwa, operation Kikwete, kikosi cha 824 kj kilichopo wilayani Kakonko mkoani Kigoma, ambapo jumla ya vijana wapatao 507mujibu wa kujitolea wamehitimu mafunzo ya awali
Aliongeza katika maeneo ya mipakani ndani ya mkoa wa kigoma, kumekuwa na tabia ya wahamiaji haramu kuingia nchini kupitia njia ambazo si halali, kitendo ambacho hupelekea wengi wao kuingia nchini na kutekeleza vitendo vya uharifu ikwemo uporaji.
Aidha kanali machibya amewasihi vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya jeshi la kujenga taifa jkt, operation Kikwete kudumisha uzalendo na mshikamano wa taifa ili kuleta maendeleo zaidi, badala ya kutanguliza mbele ubaguzi wa kidinina kabila vitendo ambacho amesema kinaweza kuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo.
Mwakiishi wa mkuu wa jeshi la kujenga taifa nchini kanali john mbungo, alisema lengo la kuwepo kwa mafunzo ya jeshi la kujenga taifa nchini, ni kuandaa malezi bora ya vijana wa kitanzania, uzalishaji mali na ulinzi wa taifa, pamoja na kuwaandaa vijana kuwa wazalendo na kuwataka vijana hao kuitumia vema nafasi hiyo.
Kaimu kamanda wa kikosi hicho, major Emanuel buliga, alisema kuwa katika kipindi chote cha mafunzo ya vijana hao, wamefanikiwa kulima hekali zipatazo 222 za alizet, kama sehemu ya kuwajengea uwezo wa uzalishaji mali ili waweze kuwa chachu ya kuchochea maendeleo katika jamii, ambapo kaimu kamanda huyo wa kikosi, ametoa wito kwa wakazi wa wilaya ya kibondo na kakonko, kujihusisha na kilimo cha alizeti, ili waweze kutumia zao hilo kiuchumi kama zao la biashara.
Hata hivyo baadhi wahitimu wa jeshi hilo, ambao ni AN 5725Abel Yohana na AN5784 SM Fotunatus Angelo, waliipongeza serikali kwa kupitia jeshi hilo kuwapatia mafunzo mbalimbali kama kilimo , ukakamavu, na namna ya kuishi katika jamii mambo ambayo wakili kuwa yamebadirisha tabia zao na kuwajenga waweze kujitegemea mahali popote watakapo kuwa
Maoni
Chapisha Maoni