Kutokana na ujio wa Wakimbizi wanaoendelea kuingia hapa nchini wakikimbia machafuko nchini Burundi, na kuingia Tanzania Mkoani Kigoma, hali hiyo imeonekana kuihathili kiutendaji katika Hospitali ya wilaya ya kibondo Mkoani humo, kutokana na mzigo mkubwa wa wagonjwa wanaofika kupata huduma ya matibabu
Kibondo Kutokana na ujio wa Wakimbizi wanaoendelea kuingia hapa nchini wakikimbia machafuko nchini Burundi, na kuingia Tanzania Mkoani Kigoma, hali hiyo imeonekana kuihathili kiutendaji katika Hospitali ya wilaya ya kibondo Mkoani humo, kutokana na mzigo mkubwa wa wagonjwa wanaofika kupata huduma ya matibabu
Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Adam Jonathan aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari hospitalini hapo juzi, alipokuwa akipokea msahada wa mashuka stini yenye thamani ya shilingi la saba na tisin elfu yaliyotolewa na shirika la umeme nchini Tanesco kwa ajili ya wodi ya wazazi
Adam aliongeza kuwa kutokana na ongezeko la watu hususa wakimbizi wanaotoka makambini hasa wajawazito wanaokuja kujifulia kwenye hospitali hiyo, kumekuwa kukisababisha uhitaji mkubwa wa vitanda, mashuka na Magodoro na miundo mbinu akiongeza kuwa kwa hivi sasa wanafanya upasuaji kwatu wanne hadi watano kwa siku tofauti na hapo nyuma ambapo ilikuwa zinapita siku mbili bila kufanya upasuaji huku kupongeza shirika hilo kwa kutoa msahada huo
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco kanda ya Magharibi Bw, Makoye Englibert alisema kuwa yeye na wafanyakazi wenzake wamewia kutoa msahada huo katika jamii iliyo katika mazingira hayo hasa kwa kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za kuisadia jamii hasa watu wanaoishi pembezon
Aidha Englibert alitoa wito kwa mashirika na Taasisi mbalimbali hapa nchini kusaidia jamii za namna hiyo hasa wakimama kwasababu wamekuwa wakikutana na hali ngumu hasa pale wanapohitaji hudu za kujifungua kama kukosekana damu za kutosha madawa katika hospitali nyingi na vituo vya afya hapa nchini
Kwa upande wa baadhi ya wanawake katika wodi hiyo ya wazazi ambao ni Feda Samweli na Angelina Kapela walipongeza shirika hilo kwa kutoa msahada na kueleza kuwa utasaidia sana maana wapo wakina mama wenzao kulinga na uwezo mdogo wamekuwa wakifika bila kuwa na mashuka au vifaa vingine stahiki mwananmke anayekwenda kujifungua kama mashuka hata kanga
Meneja Tanesco kanda ya Magaribi Bw, Englibert Makoye wa pili kushoto akikabidhi mashuka ya msahada kwa wodi ya wajawazito hospitali ya wilaya kibondo |
Feda Samweli mzazi katika wodi ya wazazi hospitali W Kibondo |
Dr Adam Jonatha kaimu Mganga mfawidhi hospitali W Kibondo |
Englibert Makoye Meneja Tanesco kanda ya magaribi |
Maoni
Chapisha Maoni