Wadau mbalimbali wilayani kibondo mkoani kigoma wakiongozana na mkuu wa wilaya hiyo Bi.Ruthi Msafiri wametoa vitu mbalimba katika shule ya msingi nengo ya watoto wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi laki nne na nusu ili kutia hamasa kwa watoto kujisomea kwa uhuru.
Ruth Msafiri Dc Kibondo akiwa na baadhi ya watoto walemavushuleni Nengo |
Nashon Amosi mwalimu katika shule ya msingi Elimu maalum Nengo Kibondo |
Ally Kombe katibu Jumhiya ya wazazi ccm W Kibondo |
Wadau mbalimbali wilayani kibondo mkoani kigoma wakiongozana na mkuu wa wilaya hiyo Bi.Ruthi Msafiri wametoa vitu mbalimba katika shule ya msingi nengo ya watoto wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi laki nne na nusu ili kutia hamasa kwa watoto kujisomea kwa uhuru.
Akizungumza
na wazazi na walezi katibu wa jumuia ya
wazazi ccm wilayani hapo Bw.Ally Gombe
amesema hatua ya kupeleka zawadi hizo ni
baada ya kuona watoto hao wakipata adha mbalimbali wawapo shuleni na hivyo kuona
umuhimu wa kuwatembelea katika njia ya kutambua haki za watoto.
Amesema
jamii haina budi kuwa na mazoea ya kuwatembelea watoto hao mara kwa mara ili kuweza
kuwafariji pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali ambazo zitawahamasisha kusoma kwa
bidii kuwafanya jisikie kuwa nao ni miongoni mwa wanajamii.
Akitoa
shukrani zake mkuu wa shule hiyo Shaban Mzenze amepongeza uamuzi huo,nakueleza
kuwa inatia faraja kwa watoto hao wanapotembelewa na watu tofauti kulingana
hali zao za ulemavu maana wote wanashinda
ndani uzio muda wote
Sambamba na
hilo, baadhi ya walimu wamesema kuwa kwa hivi sasa wanafunzi hao wanaishi
katika mazingira ambayo si rafiki wakikakabiliana na vikwazo vya kukosa vifaa
maalum vya kujifunzia hasa kwa walemavu wa macho, shule kukosa njia maalum za
kupitia walemavu kwani walemavu wa viungo ushindwa kufika eneo la kuchukulia
chakula kwani mvua ikinyesha eneo lote ujaa tope
Nae mkuu wa
wilaya ya kibondo Ruthi Msafiri akizungumza na wazazi na walimuamewataka walimu
kuwa wavumilivu wakati serikali ikifanya taratibu za kuboresha huduma za elimu
Shule hiyo
ya Nengo elimu maalum inahudumia watoto walemavu wa aina mbalimbali ikiwa ni
pamoja na utindio wa ubongo walemavu wa Ngozi,Wasiyoona, na walemavu wa viungo
Nakupongeza sana kaka kwa jitihada zako za kutuza mambo yanavyoendelea
JibuFuta