Walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma walipo katika mpango huo wengi wanashindwa kufika katika vituo vya ugawaji wa fedha jambo ambalo huchangia baadhi ya kaya kuzikosa fedha hizo zenye lengo la kuzisaidia kaya masikini kupata mahitaji muhimu.
Walengwa wa Mpango
wa Kunusuru kaya Masikini Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma walipo katika mpango
huo wengi wanashindwa kufika katika vituo vya ugawaji wa fedha jambo ambalo
huchangia baadhi ya kaya kuzikosa fedha hizo
zenye lengo la kuzisaidia kaya masikini kupata mahitaji muhimu.
ilibainika walengwa wa mpango huo walio hama vijijini
kwao na kwende kuanzisha mashamba mapya pembeni mwa Hifadhi ya Wanyama pori
Moyowosi Kigosi na Vijiji vya Kumubanga na Kumuhasha wanashindwa kufika zoezi
la ugawaji wa fedha kutokana na kukosa taarifa za ugawaji fedha.
Jumla ya kaya 119 hazikuweza kupata fedha za uhawilishaji
kwa awamu ya tatu kutokana na uendeshaji
wa shughuli za kilimo mbali na makazi ya
watu ambapo wengine 11 wamefariki dunia hali ambayo inachangia kuwepo kwa malalamiko
katika zoezi hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya ugawaji fedha katika Kijiji cha
Kisogwe kata Busunzu Bw.Yona Emmanuel Amesema Changamoto ya walengwa kuto
jitokeza siku ya ugawaji wa fedha hali
hiyo imechangia kaya lengwa kukwamisha mpango wa maendeeo ya serikali
kwa kupunguza tatizo la kumasikini wa familia na kuboresha hali ya upatikanaji
wa chakula bora kwa watoto, kupunguza utoro mashuleni na kuboresha hali ya
upatinaji wa huduma ya afya kwa watoto.
Alisema tatizo la kijografia limechangia walengwa kushindwa
kupata taarifa ya siku ya ugawaji wa fedha kwa kaya masikini katika vijiji
husika na hivyo kupelekea walengwa wengi kutopata haki yao.
“changamato kama
hii ilijitokeza hata wakati wa zoezi la undikishaji na utambuzi wa kaya
masikili jambo ambalo kaya nyingi zinakosa haki zao kutokana na kuhama hama”.
Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Busunzu Bi.Agenes Josephat amekili
kuwepo kwa tatizo hilo na kwamba licha ya jukumu lao la kutoa taarifa kwa
wananchi juu ya zoezi la ugawaji wa fedha za uhawilishaji kwa kaya masikini
lakini wanapata wakati mgumu wa kifikisha taarifa hizo kutokana na jografia
pamoja na kutoakuwa na taarifa ni wapi walengwa wamehamia kwaajili ya shughuli
zao za kilimo.
Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Wilaya ya Kibondo Bw.
Hassan Nkuro amekili kuwepo kwa changamoto hiyo na kukili kuwa katika zoezi la
ugawaji wa fedha awamu ya tatu katika kipindi cha January na February 2016
walegwa 119 hawakupata fedha zao kutoka
na kutofika katika vituo vya ugawaji wa fedha.
Alisema Wilaya ya Kibondo inajumla ya walegwa wa kaya masikini 10,254 kutoka katika
Vijiji 40 vilivyopo katika kata 13 za Wilaya hiyo ambapo fedha zilizolipwa kwa
walengwa ni shilingi Milioni
348,960,000 na kiasi kilicho rudishwa
ofisi ya TASAF makao makuu kutokana na walengwa kutofika katika vituo vya
ugawaji wa fedha hizo ni shilingi 3,440,000.
Hata hivyo Mratibu huyo ameisisitiza jamii kuzingatia masharti na maelekezo katika matumizi ya fedha hizo kwa kuwa nunulia wanafunzi sare za shule na madafri, kupeleka watoto krini na kuwapatia chakula bora pamoja na kuanzisha shughuli ndogondogo za kukuza kipato kama kufunga mbuzi na kuku wakatakao wasaidia ba
Maoni
Chapisha Maoni