Ili kuweza kuondoa kero ya umeme kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma na kuhepusha garama kubwa katika uzalishaji wa Nishati hiyo Shirika la umeme Tanesco lina mpango wa kuanzisha mradi wa kuzalisha umeme kwenye Mto Malagarasi kwa kuokoa garama kubwa za uendeshaji
Medard Kaleman Naibu waziri Nisahati Madini |
Ili kuweza kuondoa kero ya umeme kwa wananchi wa Mkoa wa
Kigoma na kuhepusha garama kubwa katika uzalishaji wa Nishati hiyo Shirika la
umeme Tanesco lina mpango wa kuanzisha mradi wa kuzalisha umeme kwenye Mto
Malagarasi kwa kuokoa garama kubwa za uendeshaji.
Sababu inayochangia garama kuwa kubwa ni mitambo ya
kuzalisha umeme iliyoko katika wilaya zote za mkoa huo inatumia mafuta ambayo
ununuliwa kwa kiasi kikubwa hku wateja wa umeme wakiwa ni wachache huku shirika
hilo likifanya kazi kwa hasara
Akiongea na waandishi wa habari, Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard
Kalemani alipokuwa wilayani juzi Febr 20
wilayani Kibondo wakati wa ziara ya
kikazi na kutembelea miradi ya umeme mkoani humo ambapo, amesema kuwa shirika
la umeme Tanesco katika Mkoa wa Kigoma linatumia shilingi million 60 kwa siku
moja hatua ambayo ni hasara ikilinganishwa na idadi ndogo ya wateja wa nishati
hiyo
Kalemani alisema kuwa mradi wa malagaras ulikuwa uanze
kutekelezwa mwaka 2009 katika eneo la Igamba 2 ila baada ya kugundulika kuwa
eneo hilo kuna vyura na konokono ambao hawapatikani Duniani na mujibu wa sheria za mazingira za umoja wa
mataifa ukaahirishwa ila sasa mradi huo utatekelezwa julay 2016 eneo la Igamba
3 ili kuweza kuwapatia wananchi umeme wa uhakika
Awali akitoa taarifa ya wilaya kwa Naibu waziri huyo, mkuu
wa wailaya ya Kibondo Bi, Ruth
Msafiri alisema
kuwa tatizo kubwa kwa watu wanaochukua Kandarasi za kufunga umeme wa Rea
kuchelewa kukamilisha kazi zao hali inayo sababisha malalamiko kwa wananchi na
kutoleta usawa katika jamii,huku naibu waziri huyo akieleza kuwa wato waliopewa
kandarasi za ujenzi wa miundo mbinu kupitia Rea, wamepewa muda ifikapo julay
mwaka huu, wawe wamekamilisha kila kitu yabaki matatizo madodomado
Sambamba na hilo, mwenyekiti wa Simon Kanguye, ambaye ni
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, alimuomba kushugulikia swala la
ufungaji wa umeme katika Taasisi mbalimbali ikiwa ni Zahati, Vituo vya
Afya,Polis na shule za sekondari ambazo zina maabara kwa ajili ya kujifunzia
sayansi na uendeshwaji wake unaitaji
Nishati ya umeme bila hivyo hazitakuwa na kazi
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameiomba serikali kupitia
shirika hilo kupunguza garama za umeme ili
hata mwenye uwezo wa chini aweze kumudu garama hizo kwa kutumia umemekama
alivyosema Chikola Staphord mkazi wa Kibondo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni