Serikali imetakiwa kuhakikisha inaboresha maslahi ya walimu hapa nchini ili mpango wa elimu bure uwe na tija kwa Watanzania na elimu bora iweze kupatikana
KAKONKO Serikali imetakiwa kuhakikisha inaboresha maslahi ya walimu hapa nchini ili mpango wa elimu bure uwe na tija kwa Watanzania na elimu bora iweze kupatikana
Wakiongea jana katika uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya miaka 39 ya Chama cha mapinduzi,mmoja wa wakazi wa kijiji cha Chulazo kata ya Nyamtukuza wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma, ambako uzinduzi huo umefanyikia kimkoa, David Bahati, alisema kuwa mpango wa serikali katika kuwaondolea wananchi mzigo mkubwa wa kusomesha watoto ni mzuri lakini ni vema walimu wakaboreshewa mazingira ili wapate moyo wa ufundishaji hasa upande wa vijijini
‘’Hivi sasa walimu wengi kulingana na mishahara midogo wameamua kuanzisha masomo ya ziada majumbani na kutoza kiasi kikibwa cha fedha shilingi elfu kumi ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha hatua ambayo inaweza kusababisha elimu kudorola kwa sababu walimu hao uenda wasionekane katika shuguli zao za kawaida mashuleni kama jitihada za makusudi zisipo fanyika alisema Bahati’’
Endrew Kamana,yeye alisema kuwa bado wananchi wanaoishi vijijini wanakabiliwa na na changamoto nyingi na kubwa kama ukosefu wa maji safi Afya,miundo mbinu ya Barabara, kilimo duni na nyinginezo japo juhudi za serikali kuhakikisha utendaji kazi unaboreka katika sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo uadilifu zinaoneka lakini mafanikio yaweza yasiwepo kwakuwa baadhi ya watu wanaotakiwa kuwasimamia wenzao ni wakujitolea hawapati malipo yoyote kama Mabarozi na wenyeviti wa mitaa huku wanaosimamiwa wakipata mishahara akihoni ni namna gani unavyoweza kumsimamia aliyeshiba huku wewe una njaa?
Hata hivyo Baadhi ya vijana wakiwakilishwa na Fadhili Juma, walizungumzia swala la ajira linaloendelea kulikumba kundi hilo kwa muda mrefu, mmoja wa vijana hao wameiomba serikali kuweka utaratibu maalum wa kuwawezesha vijana ili wapate mitaji hata kama ni kujiari fulsa ipatikane ili waweze kuondokana na hali ya kukata tamaa katika maisha
Dr Ward Kabulu mwenyekiti CCM Mkoa wa Kigoma, ambae alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, amewataka wananchi kushirikiana na serikali ya awamu ya tano, katika juhudi zake za kuleta maendeleo halisi kwa watanzania na kutotaka mambo ya haraka kwani mafanikio yana utaratibu wake na mwisho ni kufikia kinachokusudiwa
Katika swala hilo la Elimu Katibu wa ccm wilaya ya kakokonko Julias Mbwiga amesema lengo la ccm ni ni kuisimamia serikali itekeleze yale iliyoyaahidi wananchi huku akiwataka wazazi wote ambao awajawapeleka watoto kuanza kidato cha kwanza, kufanya hivyo, ili wapate haki yao ya msingi na kabla hatua kali hazijachuliwa dhidi yao
Maoni
Chapisha Maoni