Katika kuitikia juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya Watoto na wanawake wajawazito wanaokwenda kujifunguawa katika Zahanati vituo vya afya na hosipitali kote nchini jamii imetakiwa kujitoa kwa hasa na mali hata pale serikali inapokuwa haijafikisha huduma zake
Katika kuitikia juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya Watoto na wanawake wajawazito wanaokwenda kujifunguawa katika Zahanati vituo vya afya na hosipitali kote nchini jamii imetakiwa kujitoa kwa hasa na mali hata pale serikali inapokuwa haijafikisha huduma zake Wito huo umetolewa wakati wa mkutano wa uchangiaji wa miundo mbinu ya umeme katika zahanati ya Kijiji cha kumhama kata ya Bitare wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma ambapo mwananchi mkazi wa kijiji hicho aliamua kulipia milion moja baada ya kuona shida wanazozipata wanawake mara wanapofikishwa katika zahanati nyakati za usiku kwa kutumia vibatari na tochi za simu Akipokea msahada huo wa tsh milion moja Diwani wa kata hiyo Julias Kihuna amempongeza mwananchi huyo kwa moyo wa uzalendo na kusema kuwa licha ya kuwa alishachangia pamoja na wananchi wenzake ameamua ajitolee ili tatizo liweze kumalizika na wauguzi pamoja na wanaitaji huduma wasiendelee kupata shida huku muuguzi wa...