Watu wanne wametolewa wakiwa hai kutoka kwenye vifusi siku sita baada ya jumba kuporomoka katika mtaa wa Huruma, Nairobi.
Watu wanne wametolewa wakiwa hai kutoka kwenye vifusi siku sita baada ya jumba kuporomoka katika mtaa wa Huruma, Nairobi.
Watu watatu, wanawake wawili na mwanamume, wameokolewa saa chache baada ya mwanamke kutolewa kwenye vifusi na kupelekwa hospitalini.
Juhudi za uokoaji bado zinaendelea ingawa kuna wasiwasi kwamba muda wa kupata manusura wakiwa hai unayoyoma
Kwa mujibu wa Pius Masai, mkuu wa kitengo cha taifa cha kukabiliana na majanga, idadi ya waliofariki kufikia sasa imefikia 36.
Watu 136 wameokolewa wakiwa hai lakini watu 70 kufikia sasa bado hawajulikani walipo.
Siku mbili zilizopita, mtoto wa umri wa miezi sita aliokolewa baada ya kukaa kwenye vifusi kwa siku nne.
Msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kupelekwa hospitalini
Alipatikana akiwa amefunikwa kwa blanketi ndani ya ndoo na hakuonekana akiwa na majeraha yoyote.
Babake mtoto huyo, Bw Ralson Wasike, akihutubia wanahabari baadaye, alisema bintiye amekuwa na nguvu sana.
Maoni
Chapisha Maoni