Alieyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Western Tanganyika Mkoani kigoma Naftali Bikaka, alieyefariki Dunia Mei 3mwaka huu alizikwa jana wilayani Kibondo



Alieyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Western Tanganyika  Mkoani kigoma Naftali Bikaka, alieyefariki Dunia Mei 3mwaka huu alizikwa jana  wilayani Kibondo

Akiongoza mamia ya waomboleza ji Askofu Sadock Makaya,  ambaye anaongoza Dayosesi ya  Western Tanganyika kwa sasa,  kwa niaba ya Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Nchini Dr Jacob Chimeledja, alimtaja Bikaka kuwa wakati wa uhai wake alikuwa mpenda watu na alipenda kuwajenga watu katika maisha ya kujitegemea

Aidha Makaya alisema wataendelea kuyaenzi yale aliyoyafanya na kuitaka jamii kuishi kwa kutenda mema kuwasaidia maskini na kumtumania Mungu na kuishi kwa kufuata maadili ya Kiroho ili amani ya Taifa ili izidi Kudumu

Kwa upande wake Askofu wa Dayosesi ya KibondoDr Themeo Ndenza, alisema  swala la kuwasaidia watu au kuwatendea mema silazima kuwa kiongozi wa Dini yoyote ila kila mmoja sehemu alipo iwe mahala pa kazi kama ofisini au kwenye Biashara mtu anatakiwa kufanya yanayo ustaili ubinada

Hata hivyo baadhi ya waumini wa kanisa lahilo, ambao ni Christopher Chubwa na Lameck Jonas, wamesema licha ya Hayati Bikaka kufanya mema na kutangazwa wakati wa msiba wake  na kwakuwa alikuwa amestaafu aliishi maisha ya kawaida na kuonekana kama aliyesahaulika na kuutaka uongozi wa kanisa hilo kuwajali wastaafu wake kuliko kuwafanyia mazuri na mazishi ya kifahali wakati hayawasaidi kitu chochote wakiwa marehemu

Askofu Nafutali Bikaka alizaliwa jan 1947 Biturana Kibondo na alishika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa Kanisa hilo ikiwa ni pamoja na ngazi ya Askofu Dayosesi ya Western Tanganyika na baadae kugawanywa kuwa Dayosisi ya Kibondo na alistaafu mwaka 2012 kisha kufariki Mei 3. 2016 katika Hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa shinikizo la Damu ameacha mjane 1 watoto 9 na wajukuu 16

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao