Kibondo; Shule za sekondari zilizoko vijijini hapa nchini zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwaemo ukosefu wa umememe wa uhakika kwa ajili ya kuendeshea maabara licha ya serikali kutilia mkazo ujenzi wa maabara hatua inayoweza kukwamisha ndoto za wanafunzi hasa wa masomo ya sayansiWahitimu wa kidato cha sita Shule ya sekondari wasichana Bon Consilii
Wahitimu wa kidato cha sita shule ya sekondari wasichana Bon concilii Mabamba |
Dr Ibrahim Mgeni rasmi |
Janeroza Mpilirwe mkuu wa shule Bon consilii |
Kibondo; Shule za sekondari zilizoko vijijini hapa nchini zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwaemo ukosefu wa umememe wa uhakika kwa ajili ya kuendeshea maabara licha ya serikali kutilia mkazo ujenzi wa maabara hatua inayoweza kukwamisha ndoto za wanafunzi hasa wa masomo ya sayansi
Wakizungumza juzi wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Bon consilii iliyoko wilayani Kibondo mkoani kigoma katika mahafali ya 12 ya kuhitimu Kidato cha sita ambao ni Isabela Kilongozi na Irene Masabo walisema kuwa ukosefu wa umeme wa uhakika kwa shule zilizoko vijijini hawapati fulsa nzuri ya kujifunza hasa masomo ya sayansi kwakuwa maabara hizo lazima zitegeme umeme
Aidha walisema tatizo la uhaba wa walimu wa kudumu masomo ya sayansi limekuwa likiwahathili hasa pale wanapojikuta kwa mwakammoja wanafundishwa na walimu wanne somo moja ambapo kila mwalimu anakuja na mfumo
Kwa upande wao Exavel Migalambo na Gregoly Bonefas, walimu wameeleza kuwa kutokana na tatizo hilo la uhaba wa walimu ni vema serikali ikaweka utaratibu maalum wa kuwapata walimu wa kudumu mashuleni ikiwa ni pamoja na vifaa vya kufundishia
Hata hivyo mmoja wa wahitimu Juliter Mathias alisema kuwa pamoja na sekali kuweka utaratibu wa elimu bila malipo kumekuwepo na hali ya baadhi ya wazazi na wanafunzi kutotambua umuhimu huo kutokana na makundi malika na kueata wazazi walimu na jamaii kwa ujumla kutoa elimu lika ili waweze kujitambua
‘’Pamoja na kuwepo mfumo wa elimu bila malipo jamii imetakiwa kuchangia sekta pale inapo bidi na kuacha kusema kuwa serikali itafanya kila kitu licha ya kuwa watoto ni wa wazazi wenyewe’’ alisema joashi Timoth mzazi, huku mgeni rasmi Padre Andrea Pelamie akiwataka wahitimu kuwa kielelezo katika jamii kama wasomi
Maoni
Chapisha Maoni