Kibondo; Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kuungana na kushirikiana katika shuguli za maendeleo kwenye maeneo yao ili kuweza kufikia malengo yanayokusudiwa bila kuiachia serikali peke yake
Kibondo; Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya
kuungana na kushirikiana katika shuguli za maendeleo kwenye maeneo yao
ili kuweza kufikia malengo yanayokusudiwa bila kuiachia serikali peke yake
Akizungumza jana
katika kikao cha Harambee iliyoandaliwa kwa ajili ya kuchingia madawati
ya shule za msingi na sekondari Wilayani Kibondo mkoani Kigoma Bw, Philpo
Kayanda Afisa Elimu Watu wazima wa Mkoa huo, aliesema kuwa bila jamii
kushirikiana maendeleo hayawezi kupatikana
Kayanda aliongeza kuwa
watu wengi wamezoea kutoa michango mikubwa kwenye sherehe za harusi na
nyinginezo kuliko kusaidia watu wenye matatizo na shughuli za maendeleo hatua
ambayo imekuwa ikifanya mambo mengi kuzorota kwa madai kuwa serikali itafanya.
Katika harambee hiyo,
wananchi, mashirika ya umma Taasisis za serikali waliweza kutoa michango
mbalimbali ili kuziba pengo kubwa la upungufu wa madawati 11,150 huku shule za
msingi zinahitaji 17,740 na yaliyopo ni 12 elfu tu pungufu 7720 na sekondari
yanaitajika 6000 yaliyopo 3420 tu
Zoezi hilo lilionyesha
mafanikio baada ya wadau hao wa elimu kuchanga fedha tasilim tsh million
13.5 na ahadi tsh 20 milion,madawati 100 na ahadi ya madawati 6010,
huku michango yote ikitarajiwa kukamilisha april 25
Hata hivyo baadhi ya
wakazi wa kibodo,ambapo Bw, Bonefas Buyogela walipongeza jitiada za
serikali kwa kuwashirikisha katika swala hilo na kusema kuwa wanafunzi walioko
katika shule zilizoko mkoa wa kigoma hawakutakiwa kukosa madawati kwakuwa mkoa
huo una mistu mingi hivyo, upangwe utaratibu maalum wa kutumia rasilimali hizo.
Akitoa shukrani zake
mkuu wa wilaya ya Kibondo Bi Ruth Msafiri, alieleza kuwa zoezi hilo pamoja na
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya wanasiasa
kutoshiriki ipasavyo na kuwataka wote kuacha siasa katika kazi za maendeleo ili
kufikia malengo
Nao wanafunzi
walipongeza uamuzi wa serikali kuwahamasisha viongozi wa mikoa na wilaya
kuliangalia swala la ukosefu wa matawati kwani limekuwa likiwaathili kwa kiasi
kukubwa mara wanapokaa chini na wengine kubanana hali ambayo ilifanya kutokuwa
huru, na kushusha kiwango cha elimu
Maoni
Chapisha Maoni