Kutokana nakutoshirikishwa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali hapa nchini juu ya maswala yanayohusu maendeleo katika jamii hali hiyo imetajwa kuwa ni njia mojawapo inayosababisha kutofikiwa kwa malengo yanayokuwa yamekusudiwa

Kutokana nakutoshirikishwa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali hapa nchini  juu ya maswala yanayohusu maendeleo   katika jamii hali hiyo imetajwa kuwa ni njia mojawapo inayosababisha kutofikiwa kwa malengo yanayokuwa yamekusudiwa

Akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya Madiwani iliyoandaliwana mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf, mkuu wa wilaya Kibondo mkoani Kigoma Bi Ruth Msafiri aliyewakilishwa na Kaimu katibu tawala wa wilaya hiyo Bw, Moshi Husein amesema kuwa pasipokuwepo na umoja na ushirikiano katika kutatua kero za wananchi serikali itaendelea kulaumiwa pasipo sababu na hatua za kufikia malengo zitakwama

Warsha  hiyo iliandaliwa na tasaf wilaya Kibondo kwa ajili ya   kujenga uelewa juu ya shuguli zinazofanywa na Mfuko huo, juu  ya kunusuru kaya masikini katika maeneo yao ambapo mwanzoni hawakuweza kushiriki kabisana wala kuhusishwa na kazi za mpango huo ambapo Mkufunzi katika warsha hiyo Mhamed  Motomoto, aliwataka madiwani kutoa ushirikiano kwa ajili ya mpango huo

Hata hivyo Madiwani hao licha ya kuonekana kama walitengwa  wameuomba mfuko huo kushugulikia tatizo la wenyeviti wa vijiji na kamati za ugawaji fedha la kupunguza fedha za walengwa bila maelezo yoyote huku mratibu wa Tasaf Kibondo Hassan Nkulo akieleza kuwa ni makosa kukata fedha za mlengwa hata kama kuna mchango wa maendeleo katika eneo lake mpake yeye akubali kwa lidhaa yake

Kutokana na kutoshiriki kwa muda mrefu, madiwani hao amba ni Julias Kiuna na David Simon pamoja na changamoto walizokuwa wakikutananazo walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masiki wamekuwa wakiwaendea kama viongozi ila walikoza nguvu za kutatua matazo yayo na sasa wataenda kufanya kazi wanayoielewa

Simon Kanguye mwenyekiti Halmashauri ya W Kibondo

Moshi Husein Mgeni rasmi


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao