Katika kuitikia juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya Watoto na wanawake wajawazito wanaokwenda kujifunguawa katika Zahanati vituo vya afya na hosipitali kote nchini jamii imetakiwa kujitoa kwa hasa na mali hata pale serikali inapokuwa haijafikisha huduma zake

Katika kuitikia juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya Watoto na wanawake wajawazito wanaokwenda kujifunguawa   katika Zahanati vituo vya afya na hosipitali kote nchini jamii imetakiwa kujitoa kwa hasa na mali hata pale serikali inapokuwa haijafikisha huduma zake

Wito huo umetolewa  wakati wa mkutano wa uchangiaji wa miundo mbinu ya umeme katika zahanati ya Kijiji cha kumhama kata ya Bitare wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma ambapo mwananchi mkazi wa kijiji hicho aliamua kulipia milion moja  baada ya kuona shida wanazozipata wanawake mara wanapofikishwa katika zahanati nyakati za usiku kwa kutumia vibatari na tochi za simu

Akipokea msahada huo wa tsh milion moja Diwani wa kata hiyo Julias Kihuna amempongeza mwananchi huyo kwa moyo wa uzalendo na kusema kuwa licha ya kuwa alishachangia pamoja na wananchi wenzake ameamua ajitolee ili tatizo liweze kumalizika na wauguzi pamoja na wanaitaji huduma wasiendelee kupata shida huku muuguzi wa zahanati hio, Lidia manase akieleza shida wanazopata nyakati za usiku


  
Hata hivo baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wamempongeza mwananchi mwenzao aliyeamua kujitolea kwa kiwango kukibwa licha ya kupangiwa kuchanga tsh 5000/ na wenzake wakieleza kuwa hawakuwa na imani kama umeme ungeweza kufungwa katika jengo hilo kwa muda mfupi japo uchangiaji huo ulianza Nov 2016 ambapo hawakuwa hata na umeme wa nguvu ya jua



Kwa upande wake mkazi wa kijiji hicho aliyeamua kujitolea ambaye alijitambulisha kwa jina la Stansilaus Magigwa yeye amesema kuwa amehasika kutoa kiasi hicho cha tsh 1 milion baada ya kumpeleka mjamzito katika zahanati hiyo wakati wa usiku na kukuta giza huku watumishi wa afya wakihangaika kutafuta vibatari  na mara mgonjwa wake kujikuta ameumwa na mdudu Nge gizani

Nae mwenyekiti wa kijiji hicho Fred Mpabanyanga  amesema kuwa japo wakazi wa kijiji hicho walikuwa wanaendelea na kuchangia kama utaratibu waliokuwa wamejiwekea na amepatikana mfadhili huyo, nguvu zote zitaelekezwa katika nyumba za watumishi ikiwa ni mganga na wasaidizi wake ziwekewe umeme





Garama zote za kufunga  umeme katika zahanati hiyo zilikadiliwa kuwa ni shilingi million moja kiasi ambacho alikitoa mwananchi huyo na mara moja kazi ilianzakufanyika

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao