Burundi:Kutokana na hali ya usalama kwenye mipaka ya nchi za Burundi na Tanzania kulegalega kwa kushamili vitendo vya uharifu wa kutumia siraha Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imekutana na Kamati za ulinzi za mikoa ya Cankuzo, Ruyigi, Kitega nchini Burundi na kuweka mikakati ya kuzuia uharifu huo unaoendelea kugarimu maisha ya watu na mali zao

Burundi:Kutokana na hali ya usalama kwenye mipaka ya nchi za Burundi na Tanzania kulegalega kwa kushamili vitendo vya uharifu wa kutumia siraha Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imekutana na Kamati za ulinzi za mikoa ya Cankuzo, Ruyigi, Kitega nchini Burundi na kuweka mikakati  ya kuzuia uharifu huo unaoendelea kugarimu maisha ya watu na mali zao

Akiongea katika Kikao hicho kilichofanyika juzi Mkoani Ruyigi Nchini Burundi mkuu wa wilaya ya Kibondo Tanzania, Luis Bura alisema makundi ya uharifu yanayoonekana kuvuka mipaka na kufanya ujambazi kwa kufanya mauwaji yanakuwa ni tishio kwakuwa Watanzania hivi sasa hawafanyi kazi zao kwa amani na kuvitaka vyombo vya ulinzi pande zote kushirikina

‘’Makundi ya waharifu wanao tumia siraha wanaonekana kuvuka mika na kuingia nchini mwetu kuuwa watu sasa mauwaji ya raia wetu sasa basi kinachotakiwa kamati zenu na serikali kwa ujumla kuliangalia kwa umakini mkubwa jambo hili maana ni hatari sana watu wet kwa sasa hawafanyi kazi zao kwa amani kwa kuhofia kuvamiwa hata mashambani hawaendi alisema Bura’’  
Kwa upande wake  mkuu wa Mkoa wa Ruyigi Abdalah Hassan alisema ili kuwepo mafanikio katika vita dhidi ya uharifu lazima vyombo husika pande wajenge utaratibu wa kukutana kila mara ili kujadiri namna na kupeana taarifa za haraka  kushirikiana

Mkuu wa upelelezi wa Mkosa ya Jinai wilayani Kibondo upande wa Tanzania Rutatinisibwa Tibyeilwa aliitaka serikali ya Burundi kudhibiti uzagaaji wa siraha za Moto kwakuwa watu wamekuwa wakikamtwa nchini Tanzania wanapohojiwa, udai kuwa wanazinunua Burundi

‘’ Siaraha nyingi za Moto zimekuwa zikikamatwa  katika maeneo mengi ya nchi yetu mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Tabora, Mara, Dsalaam na wahusika wanapohojiwa ueleza kuwa wanazinunua huku kwenu nchini Burundi na zimekuwa zikisababisha madhala makubwa sana hivyo tunaomba mjitahidi kudhibiti hali hiyo kwa kuwa si nzuri alisema Lutatinisibwa’’   

Mkuu wa usalama wa Jimbo la Ruyigi na Cankuzo Kanal Elia Ndizigiye amekieleza kikao hicho kuwa nchi ya Burundi ilipoingia katika matatizo wahasi walikimbia na siraha nyingi zikiwemo sare za jeshi hivyo hao ndo chanzo cha uzagaaji wa siraha bila utaratibu ili kudhibiti hali hiyo lazima ufanyike mkakati maalum
Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji