Kakonko;Wachimbaji wadogo madini wa Mgodi wa Nyamwilonge wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma wametoa msahada wa mifuko 20 ya Saruji kama mchango wao akatika jamii ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa vyumba vya madarsa katika shule ya msingi Kakonko
Mkuu wa wilaya ya Kakonko mwenye shati la mistari akikabidhiwa mifuko ya saruji na katibu wa wachimbaji wadogo Omary Bakora kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Kakonko |

Akikabidhi Sauruji hiyo katibu wa wachimbaji hao,Omary Bakora, amesema kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii wameamua kuchangia ili watanzania waweze kupata elimu Bora ila ni baada ya kuona matatizo yanayoikabili sekta elimu juu ya miundo mbinu ya Madarasa na Madawati
Akipokea msaada huo wa saruji juzi alisisitiza msaada huo kukabidhiwa kwa wakati na kutumika kutatua changamoto ya madawati katika shule ya msingi Kakonko ambapo kwa sasa tayari madarasa mawili yamepauliwa kwa nguvu za wananchi na ujenzi wa madarasa mengine mawili unaendelea pamoja na ofisi ya waalimu.
“Nawashukuru sana Wachimbaji wadogo wa Nyamwironge kwa kutoa mifuko 20 kwani si haba ninaomba na wadau wengine wajitokeze kutusaidia maana bado hali haijawa nzuri japo tunajitahidi ili kuhakikisha watoto wetu wanasoma katika mazingira yanayofaa”, alisema Kanali Hosea Ndagala.
Aidha Katibu wa mgodi Omary Ramadhan Bakora alimwomba Mkuu wa Wilaya kutembelea mgodi wa Nyamwironge ili kuweza kupata nafasi ya kukutana na wachimbaji wadogo na kushiriki kwa pamoja kuchangia shughuli za maendeleo.
Meneja wa Mgodi Alestadick Rekayo ameeleza kuwa wachimbaji wanatumia nyezo duni hivyo Serikali iwasidie kuleta nyenzo kubwa zaidi na watu wenye nyenzo kubwa zaidi ili kurahisisha shughuli hiyo ya uchimbaji wa madini.
Mkurugenzi wa kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini Nyamwironge bwana Jackson Kabambo ameahidi kushirikiana na Serikali pale ambapo wachimbaji wadogo watajulishwa kuhusu miradi ya Maendeleo na kuomba kuwezeshwa zaidi kwa kuimarishiwa uwezo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Simon Mando alipokea msaada huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya na kuukabidhi kwa Afisa Elimu Msingi Mtahaba Mtahaba ambapo naye amekabidhi Katika shule ya Msingi Kakonko.
Shule ya Msingi Kakonko ina vyumba 5 tano vya madarasa huku ikiwa na wanafunzi 100 hali inayopelekea wanafunzi kuingia madarasani kwa zamu hali inayoweza kushusha kiwango cha elimu kwa wanafunzi
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni