Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kujitoa katika kuchangia huduma mbalimbali za kuokoa maisha ya wenzao kwa nyakati ambazo wao wanakuwa hawana uwezo wa kujihudumia kwa namna yoyote ile
Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kujitoa katika kuchangia huduma mbalimbali za kuokoa maisha ya wenzao kwa nyakati ambazo wao wanakuwa hawana uwezo wa kujihudumia kwa namna yoyote ile
Kutokana na hali hiyo waendesha vikipikipiki ambao ni kundi linalohitaji damu mara baada ya kupata ajali wahamasishwa kuchangia damu kwa hiari wajitokeza kwa wingi kwa ajili wananchi wenzao na akiba kwao
Akiongea jana Katika zoezi la uchangiaji damu lililofanyika mjini Kibondo Mkoani Kigoma kwa kuwahusisha waendesha Pikipiki maarufu Bodaboda mkufunzi wa mafunzo ya udereva toka shirika linalojihusisha na utoaji wa mafunzo hayo la APEC, Katema Kazwika alisema watu wengi mahospitalin wamekuwa wakipoteza maisha kabla ya wakati kutokana na kukosa huduma ambazo ziko chini ya uwezo wa binadamu
Kazwika ambae pia alimwakilisha Mkurugenzi wa shirika hilo Respicius Timanywa, katika kufunga mafunzo ya waendesha pikipiki, alisema kuwa pamoja na kampeni yao ya uhamasishaji wa wateja wao kujitolea kuchangia Damu waendesha Pikipiki wengi hasa makundi ya vijana yanakabiliwa na changamoto ya uelewa mdongo wa matumizi ya barabara na ukosefu wa fedha hali ambayo imekuwa ikisababisha ajali zisizo za lazima na kwakuwa wahanga wengi wa ajali ni madereva ndiyo maana wamekuwa wakiwashauri kuchangia damu
Nao baadhi ya waendesha Bodaboda waliobahatika kuchangia damu amba ni Damasi Lushas na Emmanuel Kanegene walisema wameamua kuchangia damu kutokana na adha wanazopata watu mbalimbali mara wanapohitaji huduma hiyo
Kwa upande wake Mteknologia Maabara wa wilaya ya Kibondo Lina Misanga, alieleseza licha ya kusaidia wahanga wa ajali damu imekuwa ni hitaji muhimu katika kusaidia wanawake wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano na kupongeza uamuzi wa wote waliojitolea kuchangia na kusema ipo changamoto kubwa ya upatikanaji wa damu kwenye hospitali nyingi hapa nchini, na katika zoezi hilo zimepatikana Unit25
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni