Chama cha walimu CWT wilayani kakonko mkoani kigoma kina idai halimashauri ya wilaya hiyo jumla ya shilingi Milioni 173,442,450 ambazo ni kutokana na uhamisho wa baadhi ya walimu,madai ya likizo, na fedha za kujikimu ambazo hawa kupatiwa kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Chama cha
walimu CWT wilayani kakonko mkoani kigoma kina idai halimashauri ya wilaya hiyo
jumla ya shilingi Milioni 173,442,450 ambazo ni kutokana na uhamisho wa baadhi ya
walimu,madai ya likizo, na fedha za kujikimu ambazo hawa kupatiwa kwa kipindi
cha miaka mitatu mfululizo.
Hayo yalibainishwa
jana na mwenyekiti wa chama cha walimu wilayani humo Tumaini Daniel alipokuwa akizungumza
kupitia kikao cha walimu wa shule za msingi na sekondari walipokutana kwa lengo
la kujadili namna bora ya kufanya ili kuendelea kuboresha hali ya ufaulu kwa wanafunzi
wa shule zilizopo katika wilaya hiyo.
Daniel alisema
madai hayo ni ya walimu wa shule za msingi na sekondary na kwamba katika halmashauri
hiyo kumekuwa na uhamisho kwa walimu usiozingatia utaratibu hali ambayo inawakatisha
tamaa katika ufundishaji ili kuendelea kuinua kiwango cha ufaulukwawanafunzi.
Hata baadhi
ya walimu Jesca Mpongo na Adrian Gaspal, walisema kuwa wamekuwa wakipigwa
tarehe mara wanapofika kuomba waweze kulipwa stahiki zao bila mafanikio kwa
muda mrefu hali waliyitaja kuwa niya kuwavunja moyo ikilinganishwa pia na
mazingira magumu ya kazi kwa baadhi yao
‘’Unakuta
mtu unahamishwa kutoka eneo moja hadi lingine ujalipwa chochote na unakokwenda
ni kugumu mazingira si rafiki ila unaamua kwenda tu kwa kuwa uliomba kazi huku
ukifuatiliwa lazima ufanye kazi kwa namna fulani ukisitizwa kuacha malalamiko
jamani hata malipo ya kuhamishwa si ni haki kwa mfanya kazi? Alisema Mpongo’’
Kwa upande
wake Afisaelimu shule za sekondari Christopha Bukombe akimwakilisha mkurugenzi wa
halmashauri hiyo alisema ombi lao atalifikisha ofsi ya mkurugenzi ili kuona namna
ya kuweza kufanya ili kutatua changamoto hizo zinazowakabili
walimu wa wilaya hiyo.
Kasuku
Bilago ambae ni Mbunge wa Jimbo la Buyungu wilayani humo hivi karibuni katika
moja ya mikutano yake alisema kuwa yapo malalamiko kwa walimu na watumishi
wengine wa halmashauri hiyo kuhamishwa kama adhabu kwa madai ya kisiasa na
kusema kuwa ni haki ya mfanyakazi kujiunga na chama chochote anachotaka na kuwataka
wafanyakazi kuacha kujihusisha na siasa mahala pa kazi kwa kufanya hivyo
ni kifume cha taratibu
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni