Kibondo;Kutokana na ujio wa wakimbizi toka nchini
Burundi na kuongezeka idadi ya watu wanofika kufanyakazi katika mashirika
ya kuhudumia wakimzi wilayani Kibondo mkoani Kigoma imedaiwa kuwa ni chanzo cha
ongezeko la maambukizi ya Virus vya ukimwi
Inadaiwa Mabinti
wengi wameanza kutoka maeneo ya vijijini na kujikusanya kwenye madangulo kwa
ajili ya kujiuza kutokana na msongamano wa watu kuwa wengi na wenye tabia
tofauti kwa ajili ya kutafuta pesa
Kutokana na hali hiyo,
kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichoketi Juzi,ambao
ni Hadija Maulid na Fales Nzobona, wameitaka serikali kupiga marufuku na
kusambaratisha maeneo yote yanayojihusisha na biasha ya matendo ya Ngono
yakiwemo Madangulo na uvaaji wa mavazi yanayosadikiwa kuchoe hali hiyo kwa
wanawake na wasichana
'' Inashangaza
wasichana kuvaa mavazi ya ajabu na wanatoroka vijijini kuja mjini pia wapo
baadhi ya viongozi wa Dini wanao wapotosha wananchi kula vyakula vya aina flani
ili watakapopimwa ugonjwa usionekane hali hii ni ni hatari sana kama
itaachiliwa na kuendelea alisema Nzobona
Mratibu wa kitengo cha
ukimwi kibondo Elizabet Ntabandi amekili kuwepo kwa ongezeko la maambukizi kuwa
awali yalikuwa asilimia 0.7 na sasa yako asilimia 1.9 na kusema kuwa
wanaendelea kuwaelimisha wananchi na kugawa mipira katika Vilabu vya pombe na
nyumba za kulala wageni
Pamoja na mambo
mengine katika kikao hicho cha baraza la madiwani wameendelea kulalamikia Idara
ya ardhi kipitia maliasili kuchelewa kutoa hati miliki za kudumu kwa makazi ya
wananchi vijini ili majengo na ardhi zao ziweze kumilikiwa kihalali kwa kuwa ni
agizo la serikali huku afisa amaliasili Fred Eliasafu akieleza kuwa tatizo
lilikuwa katika ofisi za ardhi mkoa wa kigoma kwakuwa afisa ardi mteule
alihamishwa na sasa ameletwa mwingine hivyo baada ya miezi mitatu zitakuwa
tayari
''Hati hizo kwa mujibu
wa sheria zinasainiwa na Afisa ardhi mteule wa mkoa hivyo aliyekuwepo alihamia
Dsalam na kwa kuwa ameletwa mpya tutalifanyia kazi maana tulimuhusisha alisema
anasaini za Wilaya ya Kausulu na akimaliza atanza za kwetu alisema Eliasafu''
Pamoja na kuahidiwa
kuwa tatizo hilo kumalizika baada ya miezi mitatu mwenyekiti wa halmashauri
hiyo Simon Kanguye amesema kumekuwepo na watendaji wengi kutotekeleza mambo kwa
wakati hali inayosababisha malaumu kwa wananchi na kukosa imani na
viongozi wao baada ya kusikia kauli zao
Maoni
Chapisha Maoni