Kibondo;Kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili wanawake, Jamii imetakiwa kulitazama kundi hilo kwa jicho la pekee ili kuondoa kero na kuboresha maisha yao
Kibondo;Kutokana na changamoto nyingi
zinazowakabili wanawake, Jamii imetakiwa kulitazama kundi hilo kwa jicho la
pekee ili kuondoa kero na kuboresha
maisha yao
Wanawake ndiyo wenye changamoto nyingi na
kundi hili. liko kama vile limesahaulika
lakini ndiyo wenye uthubutu katika kufanya kazi kukopa na wenye uaminifu wa kulipa fedha
kama marejesho ya fedha zinazokuwa zimechukuliwa na makundi yao na kuyataka mashirika.
taasisi za serikali na za binafisi kuyatazama makundi ya wanawake kwa Nyanja
zote
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya
wilaya Kibondo Mkoani Kigoma Juma Mnwele alipokuwa akifungua washa ya kujenga
uelewa kwa maofisa ugani na waratibu elimu ili nao waweze kuwaelekeza walengwa
wa mpango wa kusuru kaya kupitia shirika la Tasaf ili kuunda vikundi vya kuweka
akiba na kukuza uchumi wao kupitia
shirika la hifadhi ya jamii Tasaf mafunzo hayo yanafanyika mjini Kibondo
Warsha hiyo imewahusisha maafisa ugani wa
kata na na Waratibu Elimu kutoka katika
wilaya za uvinza na kibondo mkoani humo huku mkurugenzi huyo akiwataka kufanya
kazi kwa weledi wakitambua kuwa
wameaminiwa kufanya kazi hiyo hivyo na kuwataka kuepuka kuisababishia hasara
serikalip
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tasaf Taifa
aliyewakilishwa na ofisa mafunzo na
ushirikishaji Jamii Catherin Kisanga, alikili kutambua changamoto hizo na kueleza
kuwa Tasaf katika mpango wa kunusuru kaya masikini imepata mafanikio na
imweza kuzitambua kaya 1369649 na kutekeleza kazi zake katika Vijiji Mitaa na
Sheiya 9804 Tanzania bara na Visiwani
Nae
Mratibu wa kitengo cha kuinua uchumi wa kaya masikini Tasaf makao makuu Ester Kivuyo amesema wanatoa
semina kwa washiriki hawa ili wakawaelimishe walengwa namna ya kuunda vikundi
vya kuweka akiba na kwa ajili kuweka akiba na kukopeshana kwa ajili ya kujenga
uchumi ili kaya hizo ziwe na uchumi endelevu
katika maeneo yao
Baadhi ya washiriki wa maunzo yanaoendeshwa na Shirika la Tasaff yanayofanyika Wilayani Kibondo |
Juma Mnwele mkurugenzi Halmashauri Kibondo |
Ester Kivuyo, Tasaf Makao makuu |
Catherin Kisanga Tasaf Makao makuu |
‘’Walioko kwenye mpango hivi sasa ndiyo
wanaoruhusiwa kujiunga katika Vikundi hivyo na tuna waelimisha kutumia fedha
zile wanazogawiwa wakati uwwilishaji
fedha zinazotolewa kila baada ya miezi tatu na nivizuri wakazitumia vema maana
utaratibu huu una mwisho wake na
wafadhili ikitokea wasitisha misahada yao walengwa wabaki na shuguli zao kama
kawaida bila kuteteleka’’ alisema Ester
Maoni
Chapisha Maoni