 |
| Baadhi ya Wahitimu kidato cha sita 2018 shele ya Sekondari Bonconclii Mabamba |
 |
| Generoza Mpililwe Mkuu wa shule Bonconclii |
 |
| Devoter Januali mwalimu |
 |
| Oscar Daniel Mwalimu |
 |
| Lodrika Stewrt mwanaunzi |
 |
| Agripina Audax Mwanaunzi |
 |
| Fr Fransis Laswai mgeni Rasmi |
Wanafunzi wanaosoma katika shule za sekondari za Binafsi na serikali wamelalamikia hatua za baadhi ya walimu wanaoajiriwa katika shule hizo na wale wanaojitolea kwenye shule za serikali kwa vitendo vya kuhamahama hali inayosababisha kutoweza kujifunza ipasavyo
Wanafunzi hao wakiongea na Clouds Tv wakati wa Mahafali ya 16 ya kuhitimu kitado cha sita katika shule ya sekondari Bonconcilii Mabamba Kibondo mkoani Kigoma. ambapo wameeleza kuwa kila mwalimu ana namna ya ufundishaji wake hivyo anapoondoka gafla usababisha wanafunzikuanza upya kumuelewa mwalimu mpaya
Wamasema kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha wengi wao kushindwa kufanya vizuri na kuiomba serikali na wamiliki wa shule binafsi kuandaa mazingira mazuri huku baadhi ya walimu ambao ni Oscar Daniel na Devoter Januali wakisema kuwa wengi wao wamekuwa wakikimbilia ajira za serikalini kwakuwa ndo kuna mikataba ya kudumu na ajira za uhakika
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Kigoma Joseph Mlola aliyewakilishwa na Padre Fransis Laswai wa Parokia ya Kasumu amewataka wahitimu kutumia elimu wanayoipata kutoka mashule kuisaidia jamii kama wasomi na kuacha kujiunga na makundi yasiyofaa huku mkuu wa shule hiyo Generoza Mpililwe akiwataka kuwa wanyeyekevu na nidhamu ndipo watakapofanikiwa
Maoni
Chapisha Maoni