Kakonko;Imeelezwa kuwa kutokana na kukosekana kwa huduma bora kwa wazee ni moja ya sababu zinazochangia kufa kabla ya wakati
Kakonko;Imeelezwa kuwa kutokana na kukosekana
kwa huduma bora kwa wazee ni moja ya sababu zinazochangia kufa kabla ya wakati
Licha yasera
ya kuwahudumia wazee wenye umri mkubwa bado zipo changamo nyingi zinazowakabili
ikiwa ni pamoja na ukosefu wa chakula
mavazi huduma za bora afya na
kusababisha usumbufu mkubwa na manung’uniko yasiyoisha kutoka katika makundi ya
ya wazee
Mbonimpa
Bisaama ni Mwenyekiti wa chama cha Wazee wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma aliyasema
hayo jana wakati wa utoaji misaada kwa wazee 644 wa kata ya Nyamtukuza ambapo
alisema wapo wazee wengi wasiyojiweza na wengine wametelekezwa na watoto wao
hali inayopelekea kuishi katika Mazingira na magumu na wengine kufa kabla ya
wakati wao
Msaada
uliotolewa kwa walemavu wenye mahitaji maalumu ni wenye thama ya tsh milion
50.6 kutoka katika shirika lisilokuwa la kiserikali la Help Age ambao ni
Magoro, Mashat Viatu na Blanket huku
mkuu wa wilaya hiyo Kanali Hosea Ndagala akisistiza idara ya afya wilayani humo
kuhakikisha inawataia Vitambilisho ili waweze kupata huduma za afya bila
usumbufu
‘’Kama vifaa
vipo kwanini watu wanahidiwa kila mara bila utekelezaji? Tumekuwa kila
tunapofika maeneo mengi wazee wanalalamika kutopatiwa vitambulisho na kukosa
msaada wa haraka wanapofika maeneo ya kutolea huduma za afaya kwanii sasa
naagiza swala hili lifanyike haraka na madirisha kwa ajili ya kuwasaidia wazee
yawepo na yafanye kazi’’ alisema Ndagala.
Wilaya ya
Kakonko ina wazee wapatao 8000 waliokwishatambulika japo kazi ya utambuzi bado
inaendelea ili waweze kupatiwa stahiki zao kama wazee kwa kukumbukwa namna
walivyolitumikia Taifa ili na wengine kwa maleze mazuri na kuendelea
kutambuliwa michango yao na ushauri katika jamii huku mwakilishi wa shirika
laHelp Age lilitoa misada hiyo Janeth Mongi akieleza ili kufikia lengo hilo
lazima viongozi wa mitaa kata na Vijiji kushirikiana kulihudmia kundi hilo
kwani bado halijapitwa na wakati
Juma Maganga
yeye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya kakonkoaliwataka wazee hao misaada hiyo
kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa wasiuze bali watumia na kutoa taadhali ya
wanasiasa ambao wanaweza kuingiza jambo na mambo ya ya Kisiasa
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni