Wananchi wilayani kakonko mkoani kigoma wametakiwa kujitokeza katika zoezi la upuriziaji viatilifu katika majengo yao ili kukabiliana na ugonjwa wa maralia ambao umekuwa tishio kwa maisha ya binadamu
Kakonko;Wananchi wilayani kakonko mkoani kigoma wametakiwa kujitokeza katika zoezi la upuriziaji viatilifu katika majengo yao ili kukabiliana na ugonjwa wa maralia ambao umekuwa tishio kwa maisha ya binadamu
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya kakonko Kanali Hosea Ndagalla alipokuwa akizungumza na Mjini Kakonko jana kuhusiana na zoezi la upuriziaji viatilifu ambalo linaendelea katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Kanali Ndagalla amesema licha ya zoezi la upuriziaji viatirifu kuanza October 25 kumekuwa na changamoto mbalimbali kwa baadhi ya vijiji na kata ambao baadhi ya wananchi hufunga milango yao na kukataa kupuriziwa dawa na hivyo kukwamisha zoezi hilo.
Mganga mkuu wa wilaya hiyo Joseph Tutuba alisema kuwa kumekuwepo na na ongezeko la ugonjwa wa Maralia hasa katika Vijiji vinavyopakana na nchi ya Burundi ambako kulikokuwa na mlipuko wa ugonjwa huo
Tutuba alisema nivema zoezi hilo likafanyika hata kwenye makambi ya wakimbizi yaliyoko kwenye wilaya za Kakonko na Kibondo kwakuwa wakimbizi hao kule walikotoka nchini mwao ndiko kulikokuwa na tatizo kubwa la mlipuko wa ugonjwa wa Maralia na kuongeza kuwa kila wananchi 1000 wa wilaya ya Kakonko ambao wamekuwa wakipimwa kwa mwaka ni wananchi 400 ambao wamekutwa na maambukizi na wanataraji kunyizia dawa kwenye nyumba takribani 10 elf za wilaya ya Kakonko
Kwa upande wao baadhi yakazi wa Kakonko Juma Alkado Halima hussein, walipokuwa akizungumzia swala hilo amesema zoezi la upuriziaji viatirifu limekuja huku wananchi wakiwa hawajapewa Elimu kuhusu ya hasara na faida za upuriziaji na ndio sababu wengi hufunga milango yao na kuondoka wakati wa zoezi '
''Sisi ni tuko maeneo ya vijijini nilazima elimu itolewe watu waelewe maana mtu uwezi kumwambia toa vitu vyakonje ili tupulizie dawa na wengine kusumbua inatokana na mambo mbalimbali mapoke ya dini na mila na kudhwni uenda wdawa hiyo inaweza sababisha madhala mengine'' alisema Halima
|
ReplyForward
|
Maoni
Chapisha Maoni