Wahitimu wa Jeshi la akiba wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma wameiomba serikalikuwapa kipaumbele pale zinapopatikana fulsa za kiulinzi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za ajira na pia kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kijeshi ili waweze kujiendeleza na kuwa na ufanisi katika shuguli zao
Wahitimu mafunzo ya awali Jeshi la akiba wakiwa katika Gwaride wakati kufunga mafunzo ya awali |
Meja Ahmad Chande Mshauri jeshi la akiba wilaya ya Kibondo |
Wahitimu wa
Jeshi la akiba wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma wameiomba serikalikuwapa
kipaumbele pale zinapopatikana fulsa za kiulinzi kwa ajili ya kukabiliana na
changamoto za ajira na pia kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kijeshi ili waweze
kujiendeleza na kuwa na ufanisi katika shuguli zao
Baada ya
kupata mafunzo mbalimbali ya kijeshi na ulinzi na usalama na ujenzi wa Taifa
kwa nyanja mbalimbali na kulingana hali halis ya upatikanaji wa ajira na kuomba
kupatiwa mafunzo zaidi ili kuongeza uwezo zaidi katika utendaji wao wa kazi
Hayo
wameyasema katika katika lisara yao iliyosomwa na Yakin Shedrack wakati wa sherehe
ya kufunga mafunzo ya jeshi hilo iliyofanyika katika Kijiji chaa Kumhasa kata
ya Mulungu Tarafa ya Kibondo na kueleza kuwa wamejifunza mambo mengi yahusoyo
ulinzi
Kwa upande
wake Mej Ahamad Chande ambaye ni mshauri wa Jeshi hilo wilaya ya Kibondo kwa
niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Luis Bura aliyekuwa amealikwa kama mgerasm
amewataka wahitimu hao kutimiza kiapo chao kwa uaminifu ili mafunzo waliyoyapa
yaweze kuwa na maana
Aliwataka
kuwana utii na nidhamu kwani askali asiyekuwa na nidhamu hafai kulitumikia
jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anstaili kuondolewa
Nao baadhi
ya wahitimu wengine Moshi Hussein na Antifonia Cosmas waliahitidi kutimiza kiapo na kuenedeka kwa
maelekezo ya jeshi hilo na kuwashauri wale ambao hawajapitia mafunzo ya kijeshi
kwa kuwaelekeza ili wawe wazalendo
‘’Tutashirikiana
na Viongozi wetu wa serikali na kutii amri halali katika vijiji na kuwa mstari wa mbele katika shughuli za
ujenzi wa Taifa kama majanga na maendeleo’’ alisema Moshi
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni