Uboreshaji wa Elimu unahitaji ushirikiano wa pamoja
Uboreshaji wa Elimu unahitaji ushirikiano wa pamoja
Kanali Evance Malasa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko alipokuwa akizungunza kwenye hafla ya Makabidhiano ya Madawati na Vitanda vilivyolewa na Benki ya NMB |
Seka Urio Meneja wa NMB Kanda ya Magharibu |
Stephan Ndaki Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kakonko |
Wakati serikali ikiendelea kuboresha miundombinu ya Elimu Wilayani
KakonkoMkoani Kigoma, Mkuu wa Wilaya hiyo Evance Malasa ameitaka jamii
kuendelea kushirikiana na walimu ili kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi
Maendeleo mazuri ya Mtoto shuleni yanategemeana na ushirikiano wa pamoja
kati ya Mwalimu Mzazi au mlezi hivyo wasiachiwe walimu peke yao ameongeza kuwa
si vizuri kusika ufaulu Wanafunzi wa
wilaya yao unendelea kushuka kila
kukicha
Malasa aliyasema hayo juzi wakati wa hafla fupi ya kupokea Vitanda na
Madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB kwajili ya shule ya Msingi Itumbiko ambapo amesema serikali kupitia wadau wamekuna
jitiada za kuboresha elimu hivyo walimu nao hawana budi kutimiza wajibu wao ili
kufikia malengo yanayokusudiwa ikiwa ni pamoja naWazazi na walezi
wa Wanafunzi
Aidha akitoa shukrani zake kwa Benki ya NMB Kanali Malasa alisema kuwa
Sekta ya Michezo imesahaliwa na kuagiza Idara husika kulifanyikazi sula hilo
kwani ni muhimu katika maisha ya Binadamu
na uboresha afya huku akiiomba Menk ya NMB kuangalia na sekta ya Michezo
katika kufadhili vifaa vya Michezo
Benki hiyo imetoa Madawati 150 kwa ajili ya shule za Msingi Nyamtukuza,
Kiyogazi na Itumbiko ambayo imepatiwa
Vitanda 50 vyote thamani yake ni Sh 28
Milion kwa ajili ya Wanafunzi wenye Mahitaji
maalum ambapo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Benson Woko ameeleza Mikakati waliyonayo kufikia
malengo ya serikali
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio
alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo kwenda na kasi ya serikali kutoa huduma
bora ya elimu na wataendelea kufanya
hivyo kwa wilaya ya Kakonko na Mkoa mzima wa Kigoma
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Itumbiko wametoa shukrani kwa upata
Madawati na Vitanda ambavyo vitasaidia kuongeza hali ya ujifunzaji wawapo
Darasani pale wanapopunguziwa mbanano na kukaa chini
Mbunge wa Jimbo la Buyungu Aloyse Kamamba yeye licha ya kuipongeza NMB kwa
namna inavyojitoa kusaidia sekta ya Elimu hapa nchini amesema wamekuwa wakipokea
fedha nyingi kwa ajili ya kuborresha miundombinu ya elimu na sekta zingine ili kupunguza
changamoto zinazowakabili Wananchi huku akiishukuru seikali kwa jitiada hizo
Maoni
Chapisha Maoni