Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao
Maulid Jumaa Mdau wa Elimu na Mkurugenzi Ahava Sekondari alipokuwa akizungumza na wanafunzi na Wazazi wakati wa Mahafali ya pili Kuitimu Kidato cha Nne |
Frolence Samizi Mbunge wa Jimbo la Muhambwe alipokuwa akiwahutubia mamia katika mahafali ya pili kuhitimu Kidato cha nne 2023 Shule ya Sekondari Ahava iliyoko Kibondo Mkoani Kigoma |
Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao
Muhingo Mwemezi Kibondo
Wazazi kutotimiza wajibu sababu zinazopelekea Vitendo vya mmomonyoko wa
maadili kuendelea kushamili kwa Watoto na wengine kushindwa kufikia ndoto zao
Licha ya maelekezo toka kwa Serika
na Wadau mbalimbali juu ya wazazi na walezi
ambayo uwataka kutimiza wajibu wao huwaachilia watoto wao katika masuala ya starehe
bila maonyo na makaripio kwa watoto na kupelekea kushindwa masomo mwisho wa kwa
wasichana kubeba Mimba na wavulana madawa ya kulevya
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wamesema wengi
wao wamekuwa wakikwama kimaendeleo ikiwa ni pamoja na masomo kutokana na wazazi
kushindwa kuwapa malezi mazuri licha ya serikali na mashirika kuendelea
kuelimisha masuala ya malezi
Jesca Kazuzuzu na Ruth Evance ni baadhi ya Wazazi nao wanasema kuwa zipo sababu mbalimbali
zinazopelekea mmomonyoko wa maadili ikiwa ni wazazi pamoja na Watoto ,,wenyewe
,,Wazazi wengine hawako tayari kuzungunza na Watoto wao kwa kuwaelez wazi kuanzia masuala ya makuzi na kujiepusha na
makundi yasiyofaa hivyo wazazi tunatakiwa kuvunja ukimya tuwasaidie Watoto wawe
wasicha au wavulana na sababu nyingine kuvunjika kwa ndoa ambapo wazazi ukosa ushirikiano
kuwalea Vijana wao,, alisema Jesca mzazi
Akiwa Mgeni rasmi katika mahafari ya kuhitimu Kidato cha nne shule ya
sekondari Ahava Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Frolence Samizi amewataka wazazi
kuhakikisha wanawaelekeza Watoto wao kuwa na maadili hadi pale watakapo fikia muda wa kujiunga na
kidato cha tano au vyuo
Ndugu wazazi mjielewe kuwa nyinyi ndio mnaotegemewa na Vijana wenu kupata
alama nzuri za ufaulu sikitu kila mmoja ajiulize
Mtoto wako anamaliza kidato cha nne je atafika muda wa kujiunga na kidato cha tano akiwa salama?
Hata hivyo baadhi ya Wasomi wametajwa kuikatisha taamaa jamii kutokana
na mienendo isiyofaa kamaa alisema mmoja
wa Wadau wa Elimu na mkurugenzi shule ya
sekondari Ahava Maulidi Juma kwani usomi
wao unavyofikiwa inakuwa tofauti na matendo yao
Maulidi aliongeza kuwa Serikali imekuwa ikitumia garama kubwa na hasara
kutokana na wasomi wengi kutojitambua kwa kukosa uaminifu wa uwajibikaji lakini
kutokana na malezi mema na maadili ya kiroho
Alisema katika shule yake wamekuwa wakiwaelekeza watoto kuyashika maadili
ya kiroho waweze kukubalika katika mfumo wa ajira wawe na Elimu bora pamoja na maadili
mema ya kiroho, hivyo kwani watawajibika ipasavyo tofauti na watu wasiyokuwa na
maadili ya Kiroho
Inategemewa Wasomi wafanye mambo mema kulingana na wanavyodhaniwa lakini
matokeo yake ni tofauti tunatarajia watuelemishe sisi ila sivyo ilivyo kama ni magonjwa
na sababu zake tunategemea elimu kutoka kwa wasomi ila wao ndiyo wanaokwenda kinyume
na kupata madila tofauti na watu ambao hawajaenda shule mfano Mtu anafahamu madhara
ya uvutaji sigara kitaalam yeye ndiye wa kwanza kuvuta je jamii iatarajie nini kutoka
kwa makundi ya wasomi kama si kutukatisha tamaa? Mtaalam anafahamu masuala ya Ngono
nzembe ambazo husababisha Magonjwa laikini yeye ndiye mtendaji wa mambo hayo je
tutafika? Ikumbukwe kuwa yote hayo ni ukosefu wa elimu ya Kiroho alisema Maulidi
Juma
Maoni
Chapisha Maoni