DC KIBONDO AWATAKA WATENDAJI WA KATA KUTUMIA SHERIA NA MIONGOZO KUHAMASISHA WAZAZI KUCHANGIA CHAKULA MASHULENI
Aggrey Magwaza Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Steeven Janks Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kibondo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma kanali Mstaafu Agrey Magwaza amewataka watendaji wa Kata kusimamia vyema suala la uchangiaji wa chakula Cha watoto mashuleni ambapo pia amewaelekeza kutumia Sheria Kwa wazazi ambapo wanakaidi maelekezo Ameyasema hayo mara baada ya kupokea taarifa za tathimini ya utekelezaji wa hali ya lishe Kwa watoto mashuleni ambapo amesema licha ya watendaji hao kutoa taarifa hizo watoto wanaopata chakula bado ni wachache ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule za Kibondo Nao baadhi ya watendaji Nasibu Nasinu Fundi Hamiswamesema mwitikio mdogo wa wazazi umesababisha watoto wengi kushindwa kupata chakula huku baadhi ya Wazazi wakitoa sababu mbalimbali ukiwemo uchumi mdogo katika familia huku Watoto shule za Msingi ambao ni Kagina Jiles na Kassim Husein, wakieleza kuwa wanapata adha kubwa kutomsikiliza Mwalimu kutokana na kukosa chakula Wanaf...